Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
👏🏻👏🏻Maisha yamebadilika sio tena kama enzi zetu ukimaliza degree ajira unachagua.
Kwa hapa tulipo nazidi kujionea vijana wengi sana wanamaliza vyuo wakiwa vijana wadogo wenye 23 hadi 25 lakini wanakuja kujipata wakiwa 30s, hapo kati stress zinawatafuna na kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya zile ndoto za "nina vyeti ntapata ajira".
Kijana inabidi ufikirie mbali zaidi, Ajira za kitaaluma za vyuoni zipo chache, na katika hizo chache kuna connections, rushwa, n.k.
Unapokuwa chuoni kwenye likizo, muda wa kupumzika, weekends, n.k. jaribu sana uanze kupata uzoefu wa shughuli walau ambazo huwezi lala njaa, zenye kuweza kukufanya uwe self dependent.
Jifunze + ujichanganye kupata ujuzi na bodaboda, bajaji, mama ntilie, wasusi, wakulima, walimu wa tushen, vinyozi, madalali, n.k.
Hii inakufanya uwe makini pia kwenye kusevu hela za boom, pocket money na vihela unavyopata kwenye hizo mishe ukiwa na lengo la kuanza kujiajiri baada ya chuo, tayari akili unakuwa umei tune kwamba utakuwa self dependent ukimaliza chuo.
Unapoga mishe zako huku unaendelea kuomba ajira tena ukiwa tayari self dependent, ni bora zaidi.
Ukiongeza na ubunifu wako wa elimu uliyonayo unaweza kupata kipato kikubwa zaidi kufanya mambo makubwa zaidi kiasi ukasahau ajira ukawaachia hizo nafasi wenye uhitaji zaidi.