Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

umeshusha vitu saaana, kumbukumbu nzuri,mimi nilikuwa mpenzi wa ukuta! weekend yangu avelon sinema..
 
umeshusha vitu saaana, kumbukumbu nzuri,mimi nilikuwa mpenzi wa ukuta! weekend yangu avelon sinema..

Haaaaa haaaaaa

Tukumbushe Movie za Enzi hizo . . . .

Kulikuwa na New Chox; Empire; Empress na zipi zingine sijui . . . .
 
hahahahahah kibonde tena[emoji23]
 
Haaaaa haaaaaa

Tukumbushe Movie za Enzi hizo . . . .

Kulikuwa na New Chox; Empire; Empress na zipi zingine sijui . . . .
waigizaji kama fred williamson, jim kelly,mwana dada pam grier,bo sevenson, amita,hema malin,vinod,ponam walikuwa juu, sinema kama black ceaser, three the hardway,enter the dragon,black samurai,amar akbar antony,dilwale,sholay nk.
 
Dah......enzi hizo nikiwa relwe Tabora.......jamaa yangu Filipo akaniacha akahamia RTC Kagera.......kipindi ndio ule wimbo wa Sisily umetoka......acha kabisa......

Enzi hizo Supreme Fred Ndala Kasheba ndio amejiunga OSS baada ya King Kiki Kikumbi Mwanza Mpango ameondoka. Kasheba akiwa na mtindo mpya Dukuduku, nakumbuka ule wimbo, ...... Mara ya kwanza umeniomba tucheze, muziki ya kwetu siwezi kukataa, mara ya pili umerudia tena, sio kwa kucheza ila kunifinya jicho....
Uliza kwanza, kabla ya kuanza upuuzi wako bwana ee, mimi ni muke ya mtu, nimekuja kucheza, nimekuja kufurahisha mwili wangu ee, nimeshaolewa...

Vv
 
waigizaji kama fred williamson, jim kelly,mwana dada pam grier,bo sevenson, amita,hema malin,vinod,ponam walikuwa juu, sinema kama black ceaser, three the hardway,enter the dragon,black samurai,amar akbar antony,dilwale,sholay nk.

Haaaa haaaaa haaaa nimecheka kwa sauti hadi najishangaaa . . .

Really? Those were the old gold time. Will never come back now
 
Daaaah . . . kweli ulikuwa mtu wa viwanja . . . . Hawa walikuwa wanatumbuiza Silent Inn Mwenge au ili ya pale Kimara (Nimesahau jina)
 
Shimoni R chugga, sometimes 7 Floor,.....luaa intaneshno.....pia disko vumbi......na Freshaz bowl pia disko za sekondari twaletewa mademu
 
Haaaa haaaaa haaaa nimecheka kwa sauti hadi najishangaaa . . .

Really? Those were the old gold time. Will never come back now
huwezi kupata enzi hizo, hazirudi, kizazi hiki kinaona nyota tu, hakukuwa simu za mkononi,hakuna internet,hakuna matv kama sasa ila kitu kikishuka marekani hakina muda kiko dar! movie ikitoka india haina muda iko dar, tulikuwa tunapata habari za marekani,cuba na urusi ya zamani kupitia kwa vijana wa ilala( ma seamen)
 
Shimoni R chugga, sometimes 7 Floor,.....luaa intaneshno.....pia disko vumbi......na Freshaz bowl pia disko za sekondari twaletewa mademu

Haaaaa haaaa ilikuwa wapi hiyo.

Kibaha High School tulikuwa tunagiza totoz Kilakala au Vituka. Blues nyimbo za akina Lionel Richie wakati huo. Headmaster alipiga marufuku kucheza blues karibu karibu. Lazima muwe mbalimbali. Mkisogeleana anasema "Hataki Mpendane Pendane" haaaaa haaa
 
Daaaah . . . kweli ulikuwa mtu wa viwanja . . . . Hawa walikuwa wanatumbuiza Silent Inn Mwenge au ili ya pale Kimara (Nimesahau jina)

Hapana mkuu, mimi nilikuwa nifuatilia kupitia RTD enzi za David Wakati akiwa Mkurugenzi wao.

Ilikuwa ifikapo saa 9 alasiri nasikiliza kile kipindi cha Ombi Lako kilichokuwa kikiongozwa na Suleman Muhogora. Pia nilikuwa nafuatilia kupitia RTD External Service, enzi za mtangazaji nguli Stephen Lyimo.

Jumamosi kulikuwa na kipindi cha Misakato, lkn pia saa 2.30 usiku RTD Idhaa ya Biashara, Uncle J Julius Nyaisanga alikuwa na kipindi kinaitwa Philips Radio Club na kale kawimbo ka kufungulia kipindi , 'sauti safi sauti kubwa, Philips, radio club...'.

Enzi hizo nilikuwa namalizia Primary School, na nikitoka sana ni Jumamosi, tunakaa nje ya DDC Magomeni wakati bendi Juwata, au Mlimani Park wakitumbuiza.

Vv
 
Haaaaaa haaaaa haaaaa

You really made my day.

Mzee Wakati alishafariki. Nyaisanga nadhani yuko AZAM na akina Tido.

Daaaahhh Long time sana
 
Duuh wakati huo mimi niko JKT. Bila shaka Vijana wa zamani wa Kitaa watatukumbusha zaidi . . .
Mkuu umetukumbuka na sisi kwa mada hii! Miaka ya mid /late 80's high school mujini tulikuwa na raha ni raha tuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…