Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Fidelis Tungaraza:

Mlionitangulia asanteni kwa michango yenu. Nami naomba nichangie kwa sababu disco era ndiyo ulikuwa wakati wa ujana wangu. Na ndiyo kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance baada ya Break Dance sijui la kusema…Safu ya Madj wa wakati huo kwa ninaowakumbuka miye walikuwa kina Justin Kussaga (SANSUI hadi BIRIBI/CLOUDS toka Sea View mpaka Italian Club).

Eddy Sally(FM Disco), Gerald-Gerry Kotto- (Mbowe au kwa jina la utani wa wakati huo CHOONI), John Bure(Rungwe), Mehboo na Clemency/t?(Gogo Disco na Floating Bar, Africana), Abby Sykes(Blowout Disco, YMCA), Ebonite WooJack(Uptown, Disco YMCA)baada ya haya madisco mawili ndipo Sudi Mwarabu akaleta Space 1900 YMCA, Madj Gerry Kotto na Seydou.

Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj wliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.Ok Tuendelee, Msasani Beach lilikuwepo disco la Marehemu? Nassoro Born City (Nasikia alifariki mwaka jana sina uhakika).

Hapa ndiyo walipoingia kina Choggy na John Peter na baadaye Nigger J na Kalikali. Au siyo?Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco. Kwa mnaokumbuka mtaweza kukubaliana nami. Nadhani kazi ile ya matangazo ilikuwa ni ubunifu wa Mzee Fred Jimmy Mdoe na mwenziye Bwana Bakari Omari.

Jet Set hawakuwa na miziki mizuri lakini walijua kutengeneza aina ya wateja na mashabiki.Wakati wote huo Princess hotel kulikuwa na Parliament Disco la kina Joe na Eddo. Nilichokuwa nakizimia Parliament Disco ni mafunk beat waliyokuwa wanayabaruza. Halafu lilikuwa disko la watoto wa mjini sina maana mbaya katika hili lakini lilikuwa ni disco la watoto wa mjini kwa maana ya watoto wa mjini kweli.Bila kusahau Pango Disco, Rex Hotel Clock Tower na lile la Continental Hotel, Nkrumah Street.

Zama ninayoizungumzia hapa mahoteli ya ukanda wa pwani ulikuwa bado umeshikwa na mabendi isipokuwa Rungwe Oceanic kwa Dj John Bure.Yakaja madisko ya maghorofani Motel Agip na New Africa Hotel. Madisko haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho mwisho na wateja wake zaidi walikuwa vijana wapya wapya, sina maana mbaya kwa kuwaita wapya wapya. Walikuwa wapya kwa sababu hawakuwa maaluatani wa jiji wengi wao walitokea mitaa ya ushuani na attitude za kiushuani.

Kweli si kweli?Bendi zilizotamba wakati huo: Brass Construction, Con Funk Shun, Earth, Wind, and Fire, The Isley Brothers, The Jacksons, Osibisa, Ross Royce, Soul Brothers, Lakeside, Kool and the Gang, Commodores, Orchestre Veve, Super Mazembe, Le Mangelepa, TP Ok Jazz, The Parliament, Fela Ransome Kuti and Afro 70, Simba Wanyika, The Wagadugu, Bunny Mack, Third World, Zappow. Jamani, nisaidieni nimezeeka kumbukumbu inavia.

Madisko ya wakati huo miziki ilikuwa mchanganyiko lakini miziki ya Kimarekani ilikuwa ndiyo inatawala.Mziki iliyotamba You can do it, Kulukuni, Moni afinda, Shakala, Sina makosa, Let me love you, Sweet mother, Easy dance, Ladies night, Sail on, Why you wanna try me, You give me fever(Love to love you darling), What you waiting for, Shake your body down to the ground, Lift up the roof, Holding on, Love’s got me dancing on the floor,This is reggae music, Night fever, Staying alive, na mingineyo mingi.

Kwa kifupi kamaliza yote, “BC” mnatukumbusha mbali sana, kumbukumbu zenye kuleta furaha, na zile za majonzi kwa wakati ule “nilivyokuwa natoroka nyumbani kwenda Disko, mfukoni nikiwa na pesa ya kiingilio tu, sina pesa ya soda na wala sijui nitarudi vipi nyumbani” na nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa kudandia lifti za washikaji, najitayarisha kupokea viboko kutoka kwa wazazi.
Keep it up BC Mnafanya kazi ya Pongezi.JL
Pumzika kwa amani mwamba.sactus mtsimbe.mungu akibariki uko uliko
 
Back
Top Bottom