Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nae kesha farikiHaaaaaa haaaaa haaaaa
You really made my day.
Mzee Wakati alishafariki. Nyaisanga nadhani yuko AZAM na akina Tido.
Daaaahhh Long time sana
Pool side(k'njaro Hotel), Whitesands Hotel DiscoEnzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.
Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).
Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansa. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye sasa anatamba Star TV ya Mwanza akiwa na jina lake halisi ya Jacob Msungu, kwenye kipindi chake cha TV cha Roving DJ.Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.
Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.
Kwa hisani ya: MATUKIO UK: NAWAKILISHA ENZI YA MIAKA YA THEMANINI (OLD SCHOOL)
My take:
Enzi hizo miaka ya 1983-1985 nilikuwa Kibaha High School (Enzi hizo tunakula Kuku na wali). na kisha JKT Ruvu. Tulikuwa kila weekend tunakuja Down Town na akina Ray Bagenda (Nadhani yuko ardhi sasa). Sometimes tunaanza Boogie (Disko la Mchana hadi majogoo.) Mbowe Hotels, YMCA; Rungwe Oceanic; Silversends, Msasani Club nk wanahusika.
Mabingwa wa Kudance wakati huo: Akina Black Moses (RIP) and the likes. Arusha Cave Disco ilikuwa ni hatari kwa kwenda mbele.
Karibuni tukumbushane
- Tuambie wewe enzi za ujana wako ulikuwa wapi na unakumbuka nini?
- Na Je; sasa hivi ma-DJ wetu hawa waliovuma wako wapi na wanafanya nini?
- Rafiki zako wa Ujana wako wapi na wanafanya nini?
- Na vipi Madisco ya Darasa la 7 enzi hizo? Secondari? High School? Vyuo? Graduation? Freshers ball? Tiririka . . . .
Kibonde huyu wa clouds...?mimi wa shamba unanikumbusha kanda za utumbo nilipokuja kwa mjomba miaka hiyo, disko tulienda donbosko (tuliita hivyo) dj alikuwa marlon, na kibonde sijui alikuwa anahusika nn alikuwa anaharibu tu mziki na uniform zake za kino muslim!
disko lilikuwa la kufana nashangaa hujakutaja huko!
Umemsahau Chuck Norriswaigizaji kama fred williamson, jim kelly,mwana dada pam grier,bo sevenson, amita,hema malin,vinod,ponam walikuwa juu, sinema kama black ceaser, three the hardway,enter the dragon,black samurai,amar akbar antony,dilwale,sholay nk.
yeah, wametoka hood moja na marlon linje, wanamuziki na wadau wa muziki wengi wa awali wametokea donbosko hapo kulikuwa kama hii mnayoita tht kwa sasa.Kibonde huyu wa clouds...?
Mkuda.Kishtobe...
Naona umemsahau na Dj Chriss Phaby, pale msasani club,kuhusu matangazo hata 1900,nao walikuwa juu kwa matangazo, ma mchoraji wao aliyekiwa akiwa chorea matangazo ni mchagaa mmoja akiitwa Mwitori nakumbika alikuwa akiishi Sea view,nakumbuka kipindi kile madisco yote yalikuwa na grade na kuna watu ilikuwa huwezi kuwa kuta pale Continental au Keys,ila watu wa keys na continental utawakuta kote,kipindi hicho Dar ilikuwa bandari salama kweli mwanamke alikuwa almasi,ukipaki gari nje ukumbi mzima utajua wewe ndio mwenye gari.Fidelis Tungaraza:
Mlionitangulia asanteni kwa michango yenu. Nami naomba nichangie kwa sababu disco era ndiyo ulikuwa wakati wa ujana wangu. Na ndiyo kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance baada ya Break Dance sijui la kusema…Safu ya Madj wa wakati huo kwa ninaowakumbuka miye walikuwa kina Justin Kussaga (SANSUI hadi BIRIBI/CLOUDS toka Sea View mpaka Italian Club).
Eddy Sally(FM Disco), Gerald-Gerry Kotto- (Mbowe au kwa jina la utani wa wakati huo CHOONI), John Bure(Rungwe), Mehboo na Clemency/t?(Gogo Disco na Floating Bar, Africana), Abby Sykes(Blowout Disco, YMCA), Ebonite WooJack(Uptown, Disco YMCA)baada ya haya madisco mawili ndipo Sudi Mwarabu akaleta Space 1900 YMCA, Madj Gerry Kotto na Seydou.
Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj wliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.Ok Tuendelee, Msasani Beach lilikuwepo disco la Marehemu? Nassoro Born City (Nasikia alifariki mwaka jana sina uhakika).
Hapa ndiyo walipoingia kina Choggy na John Peter na baadaye Nigger J na Kalikali. Au siyo?Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco. Kwa mnaokumbuka mtaweza kukubaliana nami. Nadhani kazi ile ya matangazo ilikuwa ni ubunifu wa Mzee Fred Jimmy Mdoe na mwenziye Bwana Bakari Omari.
Jet Set hawakuwa na miziki mizuri lakini walijua kutengeneza aina ya wateja na mashabiki.Wakati wote huo Princess hotel kulikuwa na Parliament Disco la kina Joe na Eddo. Nilichokuwa nakizimia Parliament Disco ni mafunk beat waliyokuwa wanayabaruza. Halafu lilikuwa disko la watoto wa mjini sina maana mbaya katika hili lakini lilikuwa ni disco la watoto wa mjini kwa maana ya watoto wa mjini kweli.Bila kusahau Pango Disco, Rex Hotel Clock Tower na lile la Continental Hotel, Nkrumah Street.
Zama ninayoizungumzia hapa mahoteli ya ukanda wa pwani ulikuwa bado umeshikwa na mabendi isipokuwa Rungwe Oceanic kwa Dj John Bure.Yakaja madisko ya maghorofani Motel Agip na New Africa Hotel. Madisko haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho mwisho na wateja wake zaidi walikuwa vijana wapya wapya, sina maana mbaya kwa kuwaita wapya wapya. Walikuwa wapya kwa sababu hawakuwa maaluatani wa jiji wengi wao walitokea mitaa ya ushuani na attitude za kiushuani.
Kweli si kweli?Bendi zilizotamba wakati huo: Brass Construction, Con Funk Shun, Earth, Wind, and Fire, The Isley Brothers, The Jacksons, Osibisa, Ross Royce, Soul Brothers, Lakeside, Kool and the Gang, Commodores, Orchestre Veve, Super Mazembe, Le Mangelepa, TP Ok Jazz, The Parliament, Fela Ransome Kuti and Afro 70, Simba Wanyika, The Wagadugu, Bunny Mack, Third World, Zappow. Jamani, nisaidieni nimezeeka kumbukumbu inavia.
Madisko ya wakati huo miziki ilikuwa mchanganyiko lakini miziki ya Kimarekani ilikuwa ndiyo inatawala.Mziki iliyotamba You can do it, Kulukuni, Moni afinda, Shakala, Sina makosa, Let me love you, Sweet mother, Easy dance, Ladies night, Sail on, Why you wanna try me, You give me fever(Love to love you darling), What you waiting for, Shake your body down to the ground, Lift up the roof, Holding on, Love’s got me dancing on the floor,This is reggae music, Night fever, Staying alive, na mingineyo mingi.
Kwa kifupi kamaliza yote, “BC” mnatukumbusha mbali sana, kumbukumbu zenye kuleta furaha, na zile za majonzi kwa wakati ule “nilivyokuwa natoroka nyumbani kwenda Disko, mfukoni nikiwa na pesa ya kiingilio tu, sina pesa ya soda na wala sijui nitarudi vipi nyumbani” na nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa kudandia lifti za washikaji, najitayarisha kupokea viboko kutoka kwa wazazi.
Keep it up BC Mnafanya kazi ya Pongezi.JL
Naona umemsahau na Dj Chriss Phaby, pale msasani club,kuhusu matangazo hata 1900,nao walikuwa juu kwa matangazo, ma mchoraji wao aliyekiwa akiwa chorea matangazo ni mchagaa mmoja akiitwa Mwitori nakumbika alikuwa akiishi Sea view,nakumbuka kipindi kile madisco yote yalikuwa na grade na kuna watu ilikuwa huwezi kuwa kuta pale Continental au Keys,ila watu wa keys na continental utawakuta kote,kipindi hicho Dar ilikuwa bandari salama kweli mwanamke alikuwa almasi,ukipaki gari nje ukumbi mzima utajua wewe ndio mwenye gari.
Umemsahau Chris Phabby the loverEnzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.
Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).
Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansa. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye sasa anatamba Star TV ya Mwanza akiwa na jina lake halisi ya Jacob Msungu, kwenye kipindi chake cha TV cha Roving DJ.Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.
Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.
Kwa hisani ya: MATUKIO UK: NAWAKILISHA ENZI YA MIAKA YA THEMANINI (OLD SCHOOL)
My take:
Enzi hizo miaka ya 1983-1985 nilikuwa Kibaha High School (Enzi hizo tunakula Kuku na wali). na kisha JKT Ruvu. Tulikuwa kila weekend tunakuja Down Town na akina Ray Bagenda (Nadhani yuko ardhi sasa). Sometimes tunaanza Boogie (Disko la Mchana hadi majogoo.) Mbowe Hotels, YMCA; Rungwe Oceanic; Silversends, Msasani Club nk wanahusika.
Mabingwa wa Kudance wakati huo: Akina Black Moses (RIP) and the likes. Arusha Cave Disco ilikuwa ni hatari kwa kwenda mbele.
Karibuni tukumbushane
- Tuambie wewe enzi za ujana wako ulikuwa wapi na unakumbuka nini?
- Na Je; sasa hivi ma-DJ wetu hawa waliovuma wako wapi na wanafanya nini?
- Rafiki zako wa Ujana wako wapi na wanafanya nini?
- Na vipi Madisco ya Darasa la 7 enzi hizo? Secondari? High School? Vyuo? Graduation? Freshers ball? Tiririka . . . .
[emoji23] nimecheka sana maisha ni safarihahahahahah kibonde tena[emoji23]
Safari resortDaaaah . . . kweli ulikuwa mtu wa viwanja . . . . Hawa walikuwa wanatumbuiza Silent Inn Mwenge au ili ya pale Kimara (Nimesahau jina)
Bila kumsahau Franco Nero.Charles Bronson[R.I.P]
Tarzan Boy ulikuwa ni moja ya nyimbo pendwa sana kutoka kundi hilo la Baltimora. Wimbo mwingine mkali kutoka kundi hilo ni Woody Woogie.Nakumbuka Baltimora-WimboTarzan Boy (oh oh oh oh oh hoh ooooh...) nikiwa Form one 1986 tulikuwa tunacheza Funky hatari
Mie mwenyewe nimepotea njia aisee, hivi huko mbele hakuna njia ya kutokea MMU?nimekosea njia hapa