Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Safari Resort Kimara, and kila Jumatano OSS walikuwa wanapatikana Kinondoni Stereo Bar, nilikuwa sina kiingilio hivyo hukaa nje kusikilizia mambo nje ya Ukumbi
Yaah!kwa mzee Hugo kisima kuna waqt alimiliki timu ya mpira ikamshinda.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Chan sing na mwana dada angel Mao huyo alikua hatari sana.Hakuna rambo wala mfuko enzi hizo filamu nyingi cowboy hapo patamu au unamkuta Fred Williamson na ten to midnight kama sio one down two to go.
Mkuu kama nakuona majestic sinema
 
Enzi hizo Supreme Fred Ndala Kasheba ndio amejiunga OSS baada ya King Kiki Kikumbi Mwanza Mpango ameondoka. Kasheba akiwa na mtindo mpya Dukuduku, nakumbuka ule wimbo, ...... Mara ya kwanza umeniomba tucheze, muziki ya kwetu siwezi kukataa, mara ya pili umerudia tena, sio kwa kucheza ila kunifinya jicho....
Uliza kwanza, kabla ya kuanza upuuzi wako bwana ee, mimi ni muke ya mtu, nimekuja kucheza, nimekuja kufurahisha mwili wangu ee, nimeshaolewa...

Vv
Huyu Freddie Supreme au Ndala Kasheba alikuwa na gitaa lake la Nyuzi Dozeni. Nikisikiliza wimbo wa Mama Maria jinsi nyuzi zilivyopigwa wakishirikiana na Nguza Vicking ilikuwa ni burudani ya aina yake!
 
Kishtobe...
miaka ile ya 1980s wakati kuwa baharia ilikuwa dili watu walishinda pale posta ya zamani kuangalia meli. Wajapani walileta meli hii MV KISTOBE ambayo ilikuwaya ajabu kidogo kwa kuwa na engine mbele badala ya nyuma na kusababisha akina mama waliojaaliwa kuitwa vistobe. Wale watu wa Ujerumani Mashariki walikuwa na meli yao ikiitwa MV. ROSTOCK na ilikuwa na nahodha mweye roho mbaya sana na ndio asili sentensi " unanifanyia rostoki sio"

images
 
Kulikua na majumba ya sinema avalon, empress, new chox, empire, odion, drive inn then likaja starlight.. Sinema zetu za kihindi na ma actor/actress, amitabh bachan, rish and shashi kapoor, hema malini, rekha, mitchun chakraboty, etc
 
miaka ile ya 1980s wakatu kuwa baharia ilikuwa dili watu walishinda pale postaya zamani kuangalia meli. Wajapani walileta meli hii MV KISTOBE ambayo ilikuwaya ajabu kidogo kwa kuwa na engine mbele badala ya nyuma na kusababisha akina mama waliojaaliwa kuitwa vistobe. Wale watu wa Ujerumani Mashariki walikuwa na meli yao ikiitwa MV. ROSTOCK na ilikuwa na nahodha mweye roho mbaya sana na ndio asili sentensi " unanifanyia rostoki sio"

images

Daaah asante sana Mkuu. Kumbukumbu njema sana na elimu tosha kwa vijana wetu wa leo.
 
Kulikua na majumba ya sinema avalon, empress, new chox, empire, odion, drive inn then likaja starlight.. Sinema zetu za kihindi na ma actor/actress, amitabh bachan, rish and shashi kapoor, hema malini, rekha, mitchun chakraboty, etc

Haaaaa haaaaa
Ilikuwa Mkiingia picha za Kihindi lazima mlie. Very emotional.

Za Bruce Lee lazima ukitoka na wewe ujifanye Mbabe kama Bruce Lee kabla hujatiwa Mkong'oto na wababe wa Mtaani.

Ni balaaa
 
Kulikua na majumba ya sinema avalon, empress, new chox, empire, odion, drive inn then likaja starlight.. Sinema zetu za kihindi na ma actor/actress, amitabh bachan, rish and shashi kapoor, hema malini, rekha, mitchun chakraboty, etc
Ni ODEON mkuu......Umeisahauje EMPIRE na CAMEO? Halafu pale Wimpie's paliwaponza sana watoto wa shule wa kike.......ulimbo wa chipsi haukuanza leo!
 
Chan sing na mwana dada angel Mao huyo alikua hatari sana.Hakuna rambo wala mfuko enzi hizo filamu nyingi cowboy hapo patamu au unamkuta Fred Williamson na ten to midnight kama sio one down two to go.

Charles Bronson[R.I.P]
 
Dah......enzi hizo nikiwa relwe Tabora.......jamaa yangu Filipo akaniacha akahamia RTC Kagera.......kipindi ndio ule wimbo wa Sisily umetoka......acha kabisa......
Hahaha..... hata wewe umo mama?
 
Dah... uzi umenikumbusha zamani sana nikiwa dereva wa EAR nikiendesha Hippo
 
Back
Top Bottom