Vijana wanakwama baada ya masomo sababu Taasisi za Elimu ya Juu zinazalisha Wasimamizi badala ya Watendaji

Vijana wanakwama baada ya masomo sababu Taasisi za Elimu ya Juu zinazalisha Wasimamizi badala ya Watendaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Licha ya juhudi zilizofanyika, Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007) iliyofanyika mwaka 2022 imebaini kuwepo kwa vijana wenye ujuzi usioendana na mahitaji ya soko la ajira. Mathalani, vijana wengi wana sifa za viwango vya chini vya ujuzi ngumu na tepe. Takwimu za uwiano wa ujuzi wa juu uliopo ni 4.6% ikilinganishwa na mahitaji ya 12% ya nguvu kazi ya vijana, 23.1% wana ujuzi wa kati ikilinganishwa na mahitaji ya 34% na 72.3% wana ujuzi wa chini ikilinganishwa na mahitaji ya 54% (ILFS, 2021).

Miongoni mwa sababu zinazochangia hali hii ni pamoja na taasisi za elimu ya juu kuzalisha idadi kubwa ya wataalam ambao ni wasimamizi kuliko watendaji; uwepo wa mitaala ambayo haina uhusiano wa moja kwa moja na mahitaji ya soko la ajira, na vijana wengi wenye elimu ya msingi na sekondari kuingia kwenye soko la ajira bila ujuzi stahiki.

Changamoto nyingine zilizobainika ni uwepo wa fursa finyu za mafunzo ya ufundi stadi hususan kwa vijana waliopo vijijini na uratibu hafifu wa mikakati na programu za ukuzaji ujuzi miongoni mwa vijana. Hali hii inasababishwa na mikakati na programu nyingi zilizopo kujikita zaidi mijini kuliko vijijini na uwepo wa wadau wanaotekeleza programu mbalimbali kwenye maeneo yanayofafana.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, mkakati wa utekelezaji utajielekeza katika kuhakikisha nguvu kazi inapata ujuzi unaofaa na wa vitendo unaohitajika katika soko la ajira; kuongeza ubora wa elimu inayozingatia umahiri na programu za mafunzo ya ujuzi, na kukuza ujuzi wa ujasiriamali, stadi za maisha na elimu ya kuendelea kujifunza miongoni mwa vijana.

Chanzo: MKAKATI WA UTEKELEZAJI WA SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA YA MWAKA 2007 2024-2034



Asilimia 71 ya vijana wenye Umri wa Miaka 15-24 wako Mtandaoni
Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani ya UNICEF 2017: Watoto katika Ulimwengu wa Kidijitali, inabainisha kuwa mtumiaji mmoja kati ya watatu wa intaneti wana umri chini ya miaka 18. Vilevile, ripoti hiyo inabainisha kuwa, 71% ya vijana wenye umri wa miaka 15-24 wako mtandaoni, na kuwafanya kuwa kundi la umri lililounganishwa zaidi duniani kote.

Kwa kuzingatia takwimu hizo, ufikivu wa teknolojia za kidigitali unawezesha vijana kutambua anuwai kamili ya haki zao za kiraia, kisiasa, kitamaduni, kiuchumi na kijamii.

Kwa kutambua umuhimu wa vijana na mapinduzi ya kidijitali, serikali imechukua juhudi mbalimbali, ikiwemo uwekezaji katika miundombinu ya TEHAMA, ujenzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano na kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wengine kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na utekelezaji wa mpango wa kufikisha mawasiliano vijijini na maeneo ya pembezoni ambapo serikali inatarajia kusimika/ kuboresha jumla ya minara 758 kwa teknolojia ya 3G/4G yenye brodibendi katika wilaya 127, kata 713, na vijiji 1,407. Serikali pia imeanzisha Mfuko wa Ufikivu wa Huduma ya Mawasiliano kwa Wote ili kuwezesha uwekezaji wa TEHAMA katika maeneo ya vijijini na mijini yenye upungufu wa huduma za mawasiliano (Rejea Taarifa ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Mwaka 2022 (Ripoti ya WHMTH, 2022).


Taarifa za kiutawala inaonyesha kuwa pengo la mgawanyo wa kidigitali bado ni mkubwa.
Kiwango cha upatikanaji wa huduma za kidigitali ikiwemo TEHAMA kati ya kaya na watu binafsi inaonyesha kuwa, sekta hiyo inakua katika mwelekeo sahihi. Licha ya ukuaji huu, ushahidi kutoka kwenye Sensa ya Watu na Makazi, 2022 na taarifa za kiutawala inaonyesha kuwa pengo la mgawanyo wa kidigitali bado ni mkubwa. Kwa mfano, katika mtandao wa asilimia 72 ya kihamisha-data kasi, iliyotengwa kwa Tanzania, ni asilimia 45 tu inayotumika.

Umiliki na matumizi ya vifaa vya TEHAMA (simu janja, vishikwambi na ngamiza) ni wa chini sana (19%), hivyo hupunguza matumizi ya huduma ya kihamisha –data kasi. Vilevile, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi, 2022, upatikanaji na matumizi ya huduma ya TEHAMA ni mdogo miongoni mwa wanawake ikilinganishwa na wanaume katika maeneo ya mjini na vijijini; na umiliki na matumizi hafifu ya mwengoya na runinga hudunisha mawasiliano ya habari na huduma muhimu.hali hii inathibitishwa na kiwango cha umiliki na matumizi ya simu na vishikwambi, ambapo takribani asilimia 34 ya watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi wanaoishi mjini wanamiliki simu au vishikwambi ambapo kwa maeneo ya vijijini ni asilimia 9 tu.

Changamoto nyingine zilizobainishwa na taarifa ya tathmini ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa matumizi yasiyo sahihi ya TEHAMA kwa vijana yanayosababisha vijana wengi kupoteza maadili na kujihusisha na wizi na udanganyifu wa kimtandao, na vijana kutokuwa na ujuzi wa kupima usalama na uaminifu wa maudhui mtandaoni.


Vijana wanachukuliwa kama sehemu ndogo ya walengwa badala ya kuwa walengwa wakuu wanaohitaji uangalizi maalum
Katika miongozo na programu hizo, vijana wanachukuliwa kama sehemu ndogo ya walengwa badala ya kuwa walengwa wakuu wanaohitaji uangalizi maalum, msaada, matunzo na huduma. Juhudi nyingine zilizotekelezwa ni uboreshaji wa miundombinu ya afya; uanzishwaji wa Kamati ya Uongozi Ngazi ya Taifa kuhusu masuala ya lishe na utekelezaji wa programu za lishe shuleni.

Kufuatia utekelezaji wa jitihada hizo, maambukizi ya VVU kwa vijana nchini yalipungua kutoka 2.0% mwaka 2011 hadi 1.4% mwaka 2017 na mimba za utotoni kupungua kutoka 24% mwaka 2017 hadi 22% mwaka 2022 (TDHS-MIS, 2022). Licha ya mafanikio yaliyopatikana, vijana wameendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo afya ya uzazi ambapo takwimu zinaonesha kuwa, mimba katika umri mdogo zimeendelea kuwepo kwa kiwango cha 22% mwaka 2022.



Takwimu hizi zinaashiria kwamba, mimba katika umri mdogo bado ni tatizo katika jamii na linahitaji jitihada mahsusi kukabiliana nalo ili kuhakikisha kuwa, wasichana wanapata fursa za kuendelea na masomo na kupata ujuzi wa kuwawezesha kupata ajira zinazostahili (Taarifa ya SIGI, Tanzania, 2022). Vilevile, Utafiti wa Viashira na Matokeo ya UKIMWI Tanzania, 2022/2023 umebaini kuwa, kiwango cha maambukizi ya VVU kwa vijana kipo juu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.

Kwa mfano, (0.8% dhidi ya 0.3% kwa vijana wa miaka 15-19; 1.8% dhidi ya 0.9% kwa vijana wenye umri wa miaka 20-24; 3.2% dhidi ya 1.8% kwa vijana wa miaka 25-29 na 6.6% dhidi ya 2.1% kwa vijana wenye umri wa miaka 30-34).

Takwimu hizi zinaashiria kwamba, vijana hususani wasichana wanakabiliwa na hatari ya magonjwa ya zinaa zaidi kuliko wavulana. Aidha, Tathmini ya Utekelezaji wa Sera (2007) imebaini kuwa, kiwango kidogo cha maambukizi kwa vijana wa kiume kinatokana na tabia ya kutojitokeza kupima VVU na kutegemea majibu kutoka kwa wenza wao.




2.10. Uongozi na Utawala Uongozi na utawala ni miongoni mwa misingi na nyenzo muhimu katika maendeleo na uwezeshaji wa vijana. Katika kuhakikisha kwamba, masuala yanayowahusu vijana na makundi mengine yanapatiwa ufumbuzi ipasavyo, ni muhimu vijana wenyewe washiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi na kupewa fursa za uongozi badala ya kuwa watazamaji.



Hata hivyo, mifumo mbalimbali ya kisera, kisheria, kimkakati na miongozo yenye lengo la kukuza uongozi na utawala kwa vijana imeendelea kutekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wadau. Miongoni mwa mifumo hiyo ni Sera ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ya Mwaka 2009 na Sheria Sura ya 103; Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Na.16, 2004; Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410; Sheria ya Asasi Zisizo za Kiserikali Sura ya 56; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 na Sheria ya Vyama vya Kijamii, Sura ya 337. Hata hivyo, mifumo yote hii inawachukulia vijana kama sehemu ndogo ya watu badala ya walengwa wakuu wanaohitaji uangalizi maalum, usaidizi na huduma. Pamoja na jitihada zilizochukuliwa na serikali, ushiriki wa vijana katika masuala ya uongozi na utawala hususani katika ngazi za maamuzi ni wa kiwango cha chini. Hali hii inaweza kuwa inasababishwa na kukosekana kwa mwongozo wa kisera
 
Back
Top Bottom