BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Siku zote mtu kufanya jambo lisilo la kwako na kulifanya kuwa la kwako lazima utaangukia pua tu. Tangu mechi ya Jana kati ya Taifa Stars na Niger kuna kitendo kilifanywa na hawa Vijana wanaookota mipira uwanjani, walirusha mara kadhaa mipira uwanjani kwa mkupuo. Watanzania wengi walishangilia, ila wengine tuliona ile haikuwa sahihi maana inaweza kusababisha adhabu kwa timu ya Taifa na siyo utamaduni wa Watanzania.
Mbaya zaidi km nilivyosema awali, kuiga kunya kwa tembo kumeonekana ktk mechi ya Mashujaa na Mbeya City. Wakati mpira unaendelea nimeiona mpira mwingine ukirushwa uwanjani na kusababisha kusimamisha mpira ili kutoa mmoja. Tabia hii isipokemewa na TFF itakomaa na kujikuta Watanzania wanakuwa na utamaduni wa hovyo wa Waarab. Utamaduni wa Mtanzani ubaki kwa Watanzania na ule wa Waarabu ubaki kwa Waarabu.
Hawa watoto wapewe elimu. Hii mechi ya Mashujaa na Mbeya City imekumbwa na huu uhuni mara kadhaa na mechi bado inaendelea, vipi ligi ikianza.