Vijana wanaookota mipira uwanjani waswahili husema usiige kunya kwa tembo. TFF chukueni hatua tunakoelekea ni kubaya zaidi

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Siku zote mtu kufanya jambo lisilo la kwako na kulifanya kuwa la kwako lazima utaangukia pua tu. Tangu mechi ya Jana kati ya Taifa Stars na Niger kuna kitendo kilifanywa na hawa Vijana wanaookota mipira uwanjani, walirusha mara kadhaa mipira uwanjani kwa mkupuo. Watanzania wengi walishangilia, ila wengine tuliona ile haikuwa sahihi maana inaweza kusababisha adhabu kwa timu ya Taifa na siyo utamaduni wa Watanzania.

Mbaya zaidi km nilivyosema awali, kuiga kunya kwa tembo kumeonekana ktk mechi ya Mashujaa na Mbeya City. Wakati mpira unaendelea nimeiona mpira mwingine ukirushwa uwanjani na kusababisha kusimamisha mpira ili kutoa mmoja. Tabia hii isipokemewa na TFF itakomaa na kujikuta Watanzania wanakuwa na utamaduni wa hovyo wa Waarab. Utamaduni wa Mtanzani ubaki kwa Watanzania na ule wa Waarabu ubaki kwa Waarabu.

Hawa watoto wapewe elimu. Hii mechi ya Mashujaa na Mbeya City imekumbwa na huu uhuni mara kadhaa na mechi bado inaendelea, vipi ligi ikianza.
 
Hakuna haja ya kulalama, mpila tumeiga na hata baadhi ya matendo pia ktk mpila yanaigwa.

Ndiyo maana walioanzisha tabia hiyo walishinda na maisha yanaendelea nawao wakafanye huko mbeya, ndiyo kabumbu!
 
watoto wana nidham mbovu sana wale, hawana maadili ya mpira hata kidogo et na wenyewe wanamvimbia refa anawaelekeza waondoke wanagoma
hawajafundishwa maadili ya mpira
Tabia za hovyo sana. Unaweza kusema walipewa maelekezo lakini nadhani ni kuiga tu.
 
Siku zote mtu kufanya jambo lisilo la kwako na kulifanya kuwa la kwako lazima utaangukia pua tu. Tangu mechi ya Jana kati ya Taifa Stars na Niger kuna kitendo kilifanywa na hawa Vijana wanaookota mipira uwanjani, walirusha mara kadhaa mipira uwanjani kwa mkupuo. Watanzania wengi walishangilia, ila wengine tuliona ile haikuwa sahihi maana inaweza kusababisha adhabu kwa timu ya Taifa na siyo utamaduni wa Watanzania.

Mbaya zaidi km nilivyosema awali, kuiga kunya kwa tembo kumeonekana ktk mechi ya Mashujaa na Mbeya City. Wakati mpira unaendelea nimeiona mpira mwingine ukirushwa uwanjani na kusababisha kusimamisha mpira ili kutoa mmoja. Tabia hii isipokemewa na TFF itakomaa na kujikuta Watanzania wanakuwa na utamaduni wa hovyo wa Waarab. Utamaduni wa Mtanzani ubaki kwa Watanzania na ule wa Waarabu ubaki kwa Waarabu.

Hawa watoto wapewe elimu. Hii mechi ya Mashujaa na Mbeya City imekumbwa na huu uhuni mara kadhaa na mechi bado inaendelea, vp ligi ikianza.
Waarabu huwa hawana ustaarabu kabisa hawa jamaa. Hizi akili unaziona sana kwenye matches zao. Ni upumbavu tu.
 
Back
Top Bottom