Kuacha kazi ni jambo gumu sana, mtu umezoea kila mwisho wa mwezi pesa inaingia kwa uhakika, ila kiuhalisia kukomaa na ajira Ni ugonjwa wa akili kwa maana share holder wote hua hawatosheki na faida kila mwaka mnapo achieve budget kuna wapa alarm Kua kuna uwezekano wa kupata zaidi wataongeza budget, hii inafanya nguvu uliyoweka mwaka uliopita utahitaji kuweka hata mara mbili yake mwaka unaofuata na wakiona hufikii malengo wanawaza namna ya kukureplace wachukue nguvu mpya, kwa haraka haraka tulio ajiliwa tujiulize swali hili itakuaje kazi unayoipenda kweny maisha yako ikafika mahala ukaona umefika na huwezi kuacha kazi Ikatokea wenye kampuni wakaamua kufunga na kuamua ku invest kweny biashara nyingine utafanyaje? Au imetokea mkataba wako ghafla umekua terminated? Kuajiliwa kuna fanya unakua unanyenyekea sana, unajipendekeza sana inafika mahala boss wako ameongea hata kitu cha kawaida unajichekesha tuu, kama huo sio ugonjwa wa akili ni nin? Kua na elimu hakuna maana ufanye kazi za ofsini, maana yake ni kuweza ku survive katika mazingira yoyote yale kwa Kua mbunifu, unakuta mtu amemaliza chuo miaka zaidi ya 2 anahangaika tu na mabahasha hafanyi kazi hata ya karanga kisa yeye msomi akae ofsini tu na mpaka hela ya vitafunwa apewe na dada zake nyumbani huu sio ugonjwa wa akili? Vijana tufikirie kujiajili tuache kuumwa huu ugonjwa wa akili.