Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Jibu langu gumu ila ni jepesi

Twambie mkoa gani upo ili tujue cha kushauri
 
Kuacha kazi na kujiari ni kutengeneza kazi nyingne na sio kukaa bure


Hivi unafikiri ujasilia Mali umegawanyika katika sehemu ngapi mpaka uogope kuacha kazi ya wenzio na kwenda kufanya yako

Kwanza ni kuwa ukifanya utafiti wa kutosha unaweza kufanya biashara na kampuni uliacha kazi na kwenda kujiari

Natani tu mkuu
 
Mkuu nimesema hivyo ili kuonyesha kwamba hiyo huenda ikawa biashara isiyohitaji mshahara mkubwa sana. Lakini hii ni biashara inayolipa sana, hasa ukipata location yenye population kubwa ya watu. Mo anakuambia kwamba :"ukitaka kuwa tajiri wekeza kwenye matumbo ya watu". Na huu uwekezaji kwenye soko la chakula ndio umemtoa Mo kibiashara. Biashara ya chakula inalipa sana mkuu.
 
Uko sahihi;ndio maana matajiri ni wachache ukiringanisha na idadi ya masikini
 
Jana kuna member mmoja alipendekeza tusome kitabu hiki, nimeweza kukipata katika mtandao. Kwa kweli members wengine wakisome ni kitabu kizuri kinapanua uwezo wa kufikiri japo sijakisoma choke ila kwa kurasa nilizosoma, ninaamini nitafaidika sana .
 
Nina ndugu zangu Mwanza mkuu.
Unaweza kwenda mwanza ukafanya utafiti kwati ya hizi biashara

Viatu kwa kuuza kwa jumla

Nguo za watoto kuuza kwa jumla

Wewe ukawa unatoa machimbo ya hapo dar na kuzipeleka huko

Na wakati huo huo ukafanya utafiti wa nini ukitoe mwanza upeleke dar
 
Pamoja sana mkuu. Wazo lako nitalifanyia kazi kwa ufasaha.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika maamuzi haya hayaitaji kusoma mavitabu kikubwa ni kujiuliza tu uko tayari

Mafanikio ni uvumilivu, mtaani kuna shule kubwa sana ya maisha , kuna wakati mambo yangu yalikua magumu sana lakini cha kushangaza sikuwai kulala njaa

Marafiki utakaokutana nao baada ya kuacha kazi watakufunza mengi usioyajua kwenye ulimwengu wa utafutaji,

Tulikua tunajidanganya kua watu wa mtaani wanamaisha magumu nikaja kugundua kua walioko makazini ndio wanamaisha magumu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…