Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Mkuu nakushukuru sana kwa kuanzisha uzi huu maalum kwa sisi tunaotaka kuacha kazi, hasa tuliopo kwenye sekta binafsi. Huku kuna manyanyaso ya kutosha...yaani ni ubabe na utemi kwa kwenda mbele. Mtu hata ukifiwa au ukawa na kikao cha harusi au familia, hupati ruhusa ya kutoka kazini.

Hapa kazini kwangu, kuna uhakika wa nyongeza ya mshahara mnano mwezi wa 8. Nasubiri mshahara upande niende benki nichukue mkopo hata wa milioni 50 niondoke hapa UTUMWANI nikajiajiri huko uraiani. Hiki kifungo cha miaka 11 kinanitosha kabisa. Kazi gani haina weekendi wala sikukuu? Kwa ujumla naichukua sana hii kazi ya shift.

Nikishachukua mkopo wangu sitajali kama nina uzoefu wa biashara au la. Nitakachofanya nitajipa takribani muda wa wiki moja nitajifungia ndani nitafakari biashara yoyote inayoweza kuniingizia kipato cha walau Tsh 20,000 kwa siku. Hata kama ni kukaanga chipsi au mihogo nitafanya ilmradi niondoke huku utumwani mwa makaburu. Kabla ya kuanza biashara yangu hiyo nitafanya business survey, ambapo nitatembea mitaani kuangalia biashara ambazo zinalipa kwa wakati huu. Hata ikibidi kujifanya kibarua wa mtu ambaye nataka kusoma biashara yake nitafanya hivyo ilmradi nipate conclusion ya ufasaha kabla sijaingia kwenye biashara husika.

Tena utafiti ngoja niuanzie hapa kwa kuwauliza wajasiriamali wenzangu (N.B: tayari najiona kama mjasiriamali mtarajiwa). Je, ndugu zangu mlionitangulia kwenye ujasiriamali, ni biashara gani ambayo nikifanya kipindi hiki cha 'vyuma kukaza' haitaniangusha? Jamani tusiwe wachoyo wa kushirikishana taarifa kwani sisi sote adui yetu ni mmoja: UMASIKINI.

Nawasilisha
Jibu langu gumu ila ni jepesi

Twambie mkoa gani upo ili tujue cha kushauri
 
ILI UWEZE KUFIKA ELFU MOJA KATIKA KUHESABU LAZIMA UANZE NA MOJA
Ninachotaka kusema ni kuwa katika maisha kila mtu ana plan zake, na zote zina mahala pa kuanzia na kufikia. Huwezi kurukia ngazi ya tano pasipo kupitia mbili, tatu na nne. Ukichukua uamuzi wa kurukia ngazi ya tano utapasuka msamba. Hapa nimeongea kimafumbo hope wengi wamenielewa.
Cha pili Hivi kuna nchi ambayao haina masikini????
Hivi leo waote tukisema tuache kazi wote serikalini, taasisi binafsi na kwingineko na tufanye ujasiriamali!
Unafikiri nini kitatokea, muhimu kujua ni kuwa kwa mambo mengi huwa yanategemeana, shughuli huwa zinategemeana, watu huwa wanategemeana, kazi nazo zinategemeana, taasisi nazo hutegemeana.
Akili za kuambiwa changanya na zakwako hata ikibidi kopa ya mwenziwe
SO WOTE HATUWEZI KUFANANA KWA NAMNA YEYOTE ILE.
Kuacha kazi na kujiari ni kutengeneza kazi nyingne na sio kukaa bure


Hivi unafikiri ujasilia Mali umegawanyika katika sehemu ngapi mpaka uogope kuacha kazi ya wenzio na kwenda kufanya yako

Kwanza ni kuwa ukifanya utafiti wa kutosha unaweza kufanya biashara na kampuni uliacha kazi na kwenda kujiari

Natani tu mkuu
 
…..
Hata kama ni kukaanga chipsi au mihogo nitafanya
…. Mkuu hii kauli maana yake kuwa ni biashara rahisi au ngumu? Maana kuna jamaa wengi duniani wanafanya kwa kuwaiga hawa washindani wako hapa chini na mmoja yuko tayari, ukitaka kujua au kufanya research ya wanaokula mihogo na kipato chao nenda Coco Beach uangalie magari na wadhifa wao,hii biashara natamani ningeiweza. Ushauri wangu chagua au fanya biashara unayoipenda, wadau wakupe ushauri.Kwa hali ya sasa watu wanaogopa hata kuchukua mkopo wa 10M, kwa kuogopa biashara kufa, lakini mawazo yangu huu ndio wakati mzuri wa kufanya biashara.Mungu akusaidie.
McDonald's is an American fast food company, founded in 1940 as a restaurant operated by Richard and Maurice McDonald, in San Bernardino, California, United States..KFC, also known as Kentucky Fried Chicken, is an American fast food restaurant chain headquartered in Louisville, Kentucky that specializes in fried chicken. It is the world's second-largest restaurant chain after McDonald's, with 22,621 locations globally in 136 countries
Mkuu nimesema hivyo ili kuonyesha kwamba hiyo huenda ikawa biashara isiyohitaji mshahara mkubwa sana. Lakini hii ni biashara inayolipa sana, hasa ukipata location yenye population kubwa ya watu. Mo anakuambia kwamba :"ukitaka kuwa tajiri wekeza kwenye matumbo ya watu". Na huu uwekezaji kwenye soko la chakula ndio umemtoa Mo kibiashara. Biashara ya chakula inalipa sana mkuu.
 
ILI UWEZE KUFIKA ELFU MOJA KATIKA KUHESABU LAZIMA UANZE NA MOJA
Ninachotaka kusema ni kuwa katika maisha kila mtu ana plan zake, na zote zina mahala pa kuanzia na kufikia. Huwezi kurukia ngazi ya tano pasipo kupitia mbili, tatu na nne. Ukichukua uamuzi wa kurukia ngazi ya tano utapasuka msamba. Hapa nimeongea kimafumbo hope wengi wamenielewa.
Cha pili Hivi kuna nchi ambayao haina masikini????
Hivi leo waote tukisema tuache kazi wote serikalini, taasisi binafsi na kwingineko na tufanye ujasiriamali!
Unafikiri nini kitatokea, muhimu kujua ni kuwa kwa mambo mengi huwa yanategemeana, shughuli huwa zinategemeana, watu huwa wanategemeana, kazi nazo zinategemeana, taasisi nazo hutegemeana.
Akili za kuambiwa changanya na zakwako hata ikibidi kopa ya mwenziwe
SO WOTE HATUWEZI KUFANANA KWA NAMNA YEYOTE ILE.
Uko sahihi;ndio maana matajiri ni wachache ukiringanisha na idadi ya masikini
 
Great, nilishaacha kazi ya Ualimu mara mbili, nikarudi kwa kazi nyingine ila pia roho yangu inaniambia kuwa ni Lazima niache kazi ili niwe na kitu ambacho ni lasting.... kazi zina muda, kazi za watu zinazeesha, zinaleta magonjwa ya stress na kukuminya sana kufikiria nje ya box. Nashukuru kwamba nakarinia kuvuka daraja hili, sitarudi nyuma this time MUNGU anisaidie. Kuna kitabu nakisoma kipo kwenye Playstore kinaitwa THINK AND GROW RICH aaaghhhh kinanitia nguvu sana, I encourage you guys mkisome pia.

Hivi vitabu vipo vingi na vya bure
Lazima tubadilike, lazima tubadilishe our Life style, inawezakana lakini ni lazima tujikane kwanza, lazima tujishushe, lazima tuwe commited.

Thank you
Jana kuna member mmoja alipendekeza tusome kitabu hiki, nimeweza kukipata katika mtandao. Kwa kweli members wengine wakisome ni kitabu kizuri kinapanua uwezo wa kufikiri japo sijakisoma choke ila kwa kurasa nilizosoma, ninaamini nitafaidika sana .
 
Nina ndugu zangu Mwanza mkuu.
Unaweza kwenda mwanza ukafanya utafiti kwati ya hizi biashara

Viatu kwa kuuza kwa jumla

Nguo za watoto kuuza kwa jumla

Wewe ukawa unatoa machimbo ya hapo dar na kuzipeleka huko

Na wakati huo huo ukafanya utafiti wa nini ukitoe mwanza upeleke dar
 
Pamoja sana mkuu. Wazo lako nitalifanyia kazi kwa ufasaha.
Unaweza kwenda mwanza ukafanya utafiti kwati ya hizi biashara

Viatu kwa kuuza kwa jumla

Nguo za watoto kuuza kwa jumla

Wewe ukawa unatoa machimbo ya hapo dar na kuzipeleka huko

Na wakati huo huo ukafanya utafiti wa nini ukitoe mwanza upeleke dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika maamuzi haya hayaitaji kusoma mavitabu kikubwa ni kujiuliza tu uko tayari

Mafanikio ni uvumilivu, mtaani kuna shule kubwa sana ya maisha , kuna wakati mambo yangu yalikua magumu sana lakini cha kushangaza sikuwai kulala njaa

Marafiki utakaokutana nao baada ya kuacha kazi watakufunza mengi usioyajua kwenye ulimwengu wa utafutaji,

Tulikua tunajidanganya kua watu wa mtaani wanamaisha magumu nikaja kugundua kua walioko makazini ndio wanamaisha magumu zaidi
 
Hiki ni kitabu kizuri pia,..
THE IMPOSSIBLE IS POSSIBLE


By John Mason

1558417734360.jpeg
 
Back
Top Bottom