Wanajukwaa wenzangu habari, mada hii imenigusa sana ninakama mwaka mmoja sasa mtaani toka niache kazi nikiwa nimefail katika kujiajiri kwa mara hii ya kwanza wakati nipo kwenye ajira kupitia mkopo niliweza kununua bodaboda 2 ambazo ziliniingiza pesa ilinipa jeuri ya kuacha kazi nikiwa na wazo kwamba niache kazi niende kujiajiri kwa kufungua biashara hata ya kibanda lakini nilifungua saluni ya kiume licha ya kwamba biashara mpya eturn yake kwa mwanzoni ni ndogo lakini changamoto ikawa kinyozi sikudumu naye alifanya kazi kwa mwezi moja tu nikamtafuta wa pili naye alikaa mwezi wiki tu sikuwana option nikafunga na kurudisha chumba cha mtu vinginevyo kodi inanihusu, nimejifunza na naendelea kujifunza kuwa katika kutaka kujiajiri sio tu mtaji ni tatizo lakini pia usimamizi wa biashara zenyewe ni ngumu.