Mkuu Wolfpack ni kweli bila risk biashara haianzi. Ndio maana watu matajiri wenye mabiashara makubwa marekani kama kina Warren Buffet hutaka kufanya ubia kupunguza risk.
Hili naona kwa Tz, wanaoliweza ni ndugu zetu wa Kilimanjaro na wakinga. Na sijui kwanini watu hawapendi kufanya hata research na kwa Tz unaweza kumuliza mtu info ya biashara akakupa bure bila gharama au kama hapa jf. Na tatizo linguine kubwa ambalo linatufanya wa TZ wengi wakafeli lakini hayo makabila 2 yanaliweza ni supervision, kiukweli 75% ya wafanyakazi na supervisors ukimuajiri anataka matatizo ayamalize kwa mkupuo kabla hata mtaji haijarudshwa hata kama mmeuchukua bank haujarudi. Mfano biashara ya Bajaj nadhani mtaji hauzidi 10M sasa driver ukimpa aiendeshe anataka yeye pesa ya kwanza kukusanya kwa siku atoe 15,000 yake, wewe mwenye biashara upate 10,000 za mwisho kama zikibaki, kama hazikubaki basi akudanganye ndio maana wachaga wakaona bora wampee akusanye mfano 15M Bajaj iwe ya driver hapo Kiswahili kinakuwa hamna na hii ni kwa biashara nyingi, tuzidi kumuomba na Mungu na kuwashukuru wanaotoa mawazo endelevu.Ila jamani walimu wetu tuwasaidie wanafunzi kusoma vitabu na wanafunzi tujifunze kujisomea vitabu, hamna njia nzuri ya kujifunza kama kusoma vitabu , nawashukuru waliotoa vitabu humu. Kwa wastani mtu ukifanya mazoezi ya kawaida unaweza kusoma karatasi za vitabu mpaka karatasi 200 kwa siku bila kuleta shida kwenye ratiba yako kila siku.
Financial education ni muhimu, hiki ni kitu ambacho hakifundishwi mashuleni au vyuoni ni kuvpata kwenye vtabu tu. Mwanafunzi mmoja alimuuliza mwalimu, kama tuna soma ili tuje tutafute pesa baadae kuna haja gani yakusoma masomo yote haya! Kwanini msitufundishi moja kwa moja namna ya kutafuta izo pesa? In short ni watu wachache sana hufanikiwa kutoka kwenye hii system. Pia mkuu asante sana maana uli chokisema ni kweli mtupu.
NOTE: mpuuze mtu ambae unamwomba ushauri wa kibiashara alafu anakwambia higo biashara haina faida alafu ukimwangalia yeye hata pipi hajawai kuuza. Nimejifunza kuwa ni kosa sana kuomba ushauri wa kibiashara fulani mfano unampanvo wa kufungua pub, duka la nafaka au stationary alafu ushauri unaenda kuupata kwa mtu ambae ni none of the above hajawai fanya usitegemee ushauri wake ni realistic lahasha ushauri wake umebase on assumptions na ni more of ideology japo pia ni vema kumsikiliza ila upate idea pengine asemalo nikutokana pia aliyo yaona kwa wengine sasa basi baada ya hapo wale walengwa ambao wako wanapambania kombe kwwnye biashara hizo unawafuata na kuzungumza sasa hawa ndio wanatoa madini ukitoka hapo ukachanganya na ya wale watazamaji na ukachanganya na akili yako lazma utapata majibu. Saivi kuna msemo watu tunasema ooh maisha magumu biashara zinafungwa sawa ndio maisha magumu na biashara zinafungwa ila iyo sio sababu ya ww kutokufanya biashara pengine hata uyo anaesema hivo hata biashara hajui na hajawai fanya. Najua humu ndani kuna wachumi....wote tunafahamu upatikanaji wa pesa ukiwa mrahisi basi kuna tatzo kubwa sana kiuchumi ila ukiwa mgumu basi tunapelekea pengine pana unafuu au pazuri correct me if I am wrong!