Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Maambukizi mapya kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24 yamezidi kuongezaka huku wasichana wakiwa vinara katika janga hilo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Uratibu wa Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa yalifanyika jijini hapa.
Mhagama alisema taarifa za utafiti zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya VVU yanawakabili zaidi vijana wenye umri huo na kwamba yamefikia asilimia 40 huku asilimia 80 kati ya hao ni vijana wakike jambo ambalo ni hatari kwa nguvu kazi ya taifa.
Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ukiwamo wa kudhibiti Ukimwi wa mwaka 2018/19 na 2022/23. Mpango huo unalenga kupunguza maambukizi mapya ya VVU, kupunguza vifo vitokanavyo na VVU na kuhakikisha watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanaendelea kutumia dawa.
Waziri Mhagama alisema kwenye mkakati huo, serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubadili tabia kwa vijana ili kudhibiti maambukizi mapya. “Lakini pia tuna mipango maalumu ya kudhibiti maambukizi kwenye mikoa ambayo ina maambukizi makubwa ambayo yako juu ya kiwango cha kitaifa ikiwamo Njombe, Iringa, Mbeya, Kagera na Geita ambayo ipo juu ya kiwango cha kitaifa,” alisema Mhagama.
Alisema kwa sasa kuna baadhi ya mikoa ambayo imebainika kuwa na kasi kubwa ya maambukizi ikiwamo Geita, Simiyu, Manyara na Dodoma. Pia alisema serikali ina mipango maalumu ya kudhibiti maambukizi mapya kwenye maeneo yenye shughuli maalumu za uzalishaji kama vile migodi na uvuvi kwa kusambaza kondomu pamoja na kutoa elimu ya kujikinga.
IPP MEDIA