Vijana wasio na ajira waache kuiangalia Serikali, watumie YouTube kujinasua kiuchumi

Vijana wasio na ajira waache kuiangalia Serikali, watumie YouTube kujinasua kiuchumi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Youtube kuna kila kitu waweza jifunza kutengeneza mashine yeyote, waweza jifunza vitu vingi vya kukukingizia kipato. Ona hawa vijana wa Mumbai Uswahilini walioingia shindano la American GOT talents na kushinda dola Milioni Moja.

 
Easy said than done. Serikali ina watu asiojua mambo mengi. Mfano mpaka leo njia ambazo vijana wangetumia kufanya biashara na kazi mtandaoni kama Paypal Tanzania BOT wana policies ambazo haziruhusu kupokea pesa.

Kenya paypal unapokea na kuwithdraw pesa kwa safaricom mpesa, Kenya hata upwork mtu ana withdraw pesa wka safaricom hata skrill pia. Yani kama kuna jambo linanishangaza Tanzania ni hili. TUko nyuma kwa vitu vingi sana sana sanaa.
 
Huwezi pata pesa Kama huna pesa.

Sera zao ni nzuri zinawainua watu. Zetu ni kuwafanya watu wawe masikini ili watawaliwe. Hakuna mjamaa au mkomunisti yeyeto duniani mwenye confidence ya kuongoza watu walioshiba only masikini na wanyonge (futereless people)
 
"Aliyeshiba hamjui mwenye njaa"

Wewe waambie ndugu zako maneno yako matupu hayo yasiyo na uelekeo.

Na serikali yako iangalie youtube ili iendelee kama china na marekani..

Jishikilie ushije onekana hamnazo mwepesi ulikosa thamani kwa jamii
 
Mtoa mada amekula na kuvimbiwa mishuzi inamtoka anawatukana wasio na Ajira. Nakumbuka ya Kigwangwala.
 
Mtoa mada amekula na kuvimbiwa mishuzi inamtoka anawatukana wasio na Ajira. Nakumbuka ya Kigwangwala
Ulitaka aseme Nini
Utakaa utegemee ajira ya serikalini mpaka lini
Unaacha kujifunza kazi mbalimbali ambazo ziko ndani ya uwezo wako kujipatia kipato unasubiri kuajiriwa
Nyie ndio hata mkiajiriwa huko makazini Hanna faida Wala hamuendi kuwa wabunifu

Mnaenda kuwa watu was kulalamika tuuuuuuuu
 
Ulitaka aseme Nini
Utakaa utegemee ajira ya serikalini mpaka lini
Unaacha kujifunza kazi mbalimbali ambazo ziko ndani ya uwezo wako kujipatia kipato unasubiri kuajiriwa
Nyie ndio hata mkiajiriwa huko makazini Hanna faida Wala hamuendi kuwa wabunifu

Mnaenda kuwa watu was kulalamika tuuuuuuuu
Hujui ulisemalo wewe.
7+7= 14+4=18+3=21
Huo ndiyo mfumo wetu wa elimu.
Hivyo vitu vipya unajifunza lini na unasoma lini?
Wanafunzi wanakaririshwa kufaulu mitihani huo ubunifu unatoka wapi????
 
Waambie watoto wote wa viongozi waliopata ajira serikalini, watoke wakaangalie hiyo youtube ili waendeleze maisha yao.
 
Serikali yenu haitaki watanzania wajipe ajira, hakuna mazingira wezeshi. Bandwidth ni gharama, hairuhusu kupokea pesa kwa PayPal, gharama za Posta ziko juu, nk.
 
Jamani tusishupaze shingo kiasi hicho kupinga kupinga simu zina mambo mengi kuna ujuzi mwingi wakuuchukua na sio lazima uwe una hela ndio uvione vinamaana au vinakupa hela unaweza soma kwa kusolve matatizo yako mwenyewe na mwisho wa siku ukasolve na ya wengine, simu ya laki moja unaacces youtube, google maps, google earth, pdfdrive, healthonline, wikihow, wikipedia na n.k kwa bando la 1000 mtoa mada ameleta chachu tu hututakiwi kumbeza hizi simu hizi kila akitumia kwa uchanya tunaweza songa mbele sana
 
Hao vijana wacheki tena wamekuwa wakishinda dola hizo milioni moja kila mwaka ona walichofanya kingine

For what I know, kwa sababu nimekuwa nikifuatilia AGT kwa muda mrefu, V.Unbeatable mwaka jana hawakushinda bali walishinda mwaka kwenye mchuano wa mabingwa... sasa hizo za kila mwaka unazotaja wewe ni zipi?!

Anyway, but that's not the case... hivi umeshawahi kujiuliza ni namna gani Vijana ambao walianza kujiari kupitia YouTube walivyokuwa wamerudishwa nyuma na serikali yako unayoitetea hapa kila wakati baada ya kuwataka walipie leseni ya eti kuwa ni Online TV wakati these are just YouTube Channel?!
 
Back
Top Bottom