Vijana wasomi msio na ajira maisha hayapo Bongo tu. Unaweza kuzamia nchi jirani ukaishi vizuri. Dunia yote ya Mola mipaka ipo ili kuleta utulivu

Vijana wasomi msio na ajira maisha hayapo Bongo tu. Unaweza kuzamia nchi jirani ukaishi vizuri. Dunia yote ya Mola mipaka ipo ili kuleta utulivu

Nikiwa na ujuzi wa udereva nie nchi gani tofauti na SA?
Hello!
Huu ndio ukweli kuwa vijana wasomi wa Zanzibar hawana changamoto ya ukosefu wa ajira kama ilivyo vijana wa Tanganyika a.k.a bara.

Vijana ombeni kibali cha ukaazi wa Zanzibar, wengine nendeni Gado(Msumbiji) kuna fursa kedekede, Msumbiji kuna amani kwa 98 %, ni sehemu ndogo tu ndio iko hovyo baada ya IS kuweka kambi.

Kuna Angola maisha yako njema.

Botswana pesa nje nje.

Siwashauri muende huko Ng'ambo kwa wazungu ambako kuna upweke mkubwa.

Fundi yeyote nenda Angola utanishukuru.

Daktari, muuguzi, watu wa maabara n k nendeni Botswana.

Wanasheria , walimu nendeni Msumbiji.

Wafanyabishara nendeni Zambia.

Wahandisi nendeni South Africa.
 
Watu hutoka kutokana na maslahi, hapa nyumbani maslahi bado kidogo kutokana na huduma ile inatolewa kwa madereva. Huko Zimbabwe wanakuja bei gani kwa mwezi? Maana kule Marekani dereva malori analipwa dollar 3 kwa maili 1 kimbembe kipo kufika huko.
Zimbabwe nenda kasukume malori.
Ila kada ya madereva Tanzania bado uhitaji upo mkubwa ushindwe wewe tu
 
Walimu wakienda Msumbiji watafundisha nini? mana Msumbiji wanatumia Kireno na huku Tanzania tunatumia Kiingereza na Kiswahili
 
Botswana Kuna uhutaji mkubwa sana wa madaktari na walimu, lkn husikii hata balozi zetu zikiweka Utaratibu wa kuuwezesha wahitimu kwenda kuchukua kazi huko. Nadhani wanaogopa lawama, kwasabb wanafahamu kuwa elimu yetu inatotoa wahitimu ambao ni half cooked.
Sio kweli mkuu Botswana,Zambia na Zimbabwe zilikua na Wafanyakazi wengi kutoka Tanzania mpaka sasa hivi wapo wachache kutokana na wao kubadili sheria za kazi kwa Wageni hapo Hwange ,Zimbabwe mkuu wa Polisi pale ni Mtanzania/Mzimbabwe na wao wanajua ana mke Mzimbabwe mtu wa Mbozi hapo watu wengi wamemfahamu wakipata matatizo yeye ndio nguzo yetu kule..nina list nyingi wacha niishie hapa kama utaelewa..
 
Back
Top Bottom