Vijana Watafuta Kadi za Uanachama wa CCM Kama Dhahabu

Vijana Watafuta Kadi za Uanachama wa CCM Kama Dhahabu

Sio wote wanachukua kadi kwa hiari, ukiachilia mbali suala la kuchukua kadi kwa fursa na maslahi binafsi.
Kwa sasa kupata kadi kuna namna tatu au zaidi, nitaelezea mbili zisizo za hiari au kizalendo.
1.Kuchukua kadi ili upate nafasi, cheo, au wadhfa fulani, hili linaangukia kwenye kundi kubwa la vijana ili kupata maslahi yao binafsi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikumba nchi yetu.
2.Kupewa kadi kwa shinikizo au kulazimishwa, mmefika mahali mna force kuwapa watu kadi bila idhini wala uhitaji wao.
Najua utakataa tu na hili, maana nimesoma maoni mengi uliyoandikiwa hapa umeshupaza shingo hautaki kusikia ( nawajua sana ).
Sasa nakuuliza swali na ujijibu mwenyewe, kwenye jamii zetu kuna watu ni wanufaika wa mpango wa kuwainua kiuchumi ( tunaujua sote ), kuna shughuli wanapewa za kufanya ili kusaidia kama kulima na kukwetua nyasi kwenye barabara za vumbi mitaani ( sijui kama huu mpango upo mikoa yote ), sasa watu tunashangaa kuona uandikishaji wa kadi kwa hao watu bila uhitaji wao. Kuna wanafaika ni wazee, wasiojiweza, au wagonjwa, hivyo wanawaagiza watoto au ndugu zao wanaoweza kufanya kazi kwenye shughuli hizo wanashangaa kukutana na mambo hayo ya lazima, sasa kijana wa miaka 18+ ukamlazimishe kadi anapeleka wapi?, huo ndio uzalendo wa vijana kuzitafuta kadi kama dhahabu?,
Mpenda Haki na Uzalendo wa kweli.
Vijana wanachukua kadi kwa hiyari Yao kutokana na kuvutiwa na Sera na ajenda pamoja na itikadi ya CCM ambazo zinagusa maisha yao ya kila siku,wametambua kuwa Ni CCM pekee yenye uchungu na maisha yao na yenye majibu ya kero na changamoto zao,ndio maana ya kuamua kujiunga CCM
 
Back
Top Bottom