Kuna siku nilikuwa naanza kazi sehemu US, nikamkuta jamaa ana tattoo kama mwili mzima, tena zile za marangirangi.
Halafu jamaa mtu poa tu.
Alikuwa anafanya kazi za web design.
Nikasema huyu mtu atakuwa na kipaji sana cha mambo ya design, halafu anayapenda sana mpaka kaamua kuufanyia mwili wake wote design za tatoo.
Na waajiri wake wamemuelewa na kumuajiri kwa kipaji chake, bila kujali anavyoonekana.
Hili ni moja kati ya mambo yanayotuangusha Africa. Tunaangalia nje mtu anaonekanaje kuliko uwezo wa mtu.
Matokeo yake, tunaacha kuchukua watu wazuri wenye vipaji ambao wana tattoo, tunakuja kuchukua wezi wasiojua kazi wanaojua kuvaa suti nzuri.
Halafu, tukishindwa kuendelea, tunashangaa kwa nini hatuendelei