Ndgu ulitakalo haliwezi kua.
Kama nilivyosema awali, kuna sekta za kufanya hayo sio sekta zote.
Wewe ulitolea mfano marekani na mimi nikafanya hivyo hivyo kua hata huko unalikosema huyo web designer aliajiliwa nako bado, ila sasa hivi tena nako unakupondea wakati kabla ulitunanga watz ukawajaza US hadi mfano ukatoa wa huko US.
Appearence ni mojawapo ya communication skills, kabla hatujaongea kwanza ni jins unavyoonekana ndio itadetermine upewe salamu ya namna gani, hapo pia ushamjudge mtu kwa muonekano wake.
Ingekua hivyo utakavyo wewe sijui kama dunia ingekalika, imagine unamkuta mtu kavaa kama Lil Wayn ndo meneja wa benki, wafanyakazi ni kama kina Ngoma nagwa na vipini vyao puani ndio wafanyakazi wa hapo, bila shala muonekano wao utaathiri mwenendo wa kampuni.
Your objection is very arbitrary, shallow and limited to what is while ignoring what could be. Basically it is rich with the poverty of imagination.
Yani ungeishi kwenye Tanzania ambayo haina barabara za lami, ungesema Tanzania haiwezi kuwa na barabara za lami, kwa sababu hujazoea kuona barabara za lami.
It is said that a revolution may seem impossible before it happens, but inevitable after it happens.
Kwanza kabisa, hakuna ninalolitaka liwe.
Nafanya uchambuzi wa abstract tu kwamba ukifanya hivi, usitegemee matokeo haya.
Kama unalima kwa kutotumia shamba lako lote na hesabu za kuvuna optimum, usitegemee mavuno optimum.
Africa ina changamoto kubwa ya ku develop na kutumia human capital. Hatujui kuangalia potential ya mtu na kui cultivate. Tunapenda sana kuweka vikwazo vya kijinga kila sehemu. Tunapenda sana kuwindana na kubwengana.
Hata malezi yetu ya watoto ni hivyo hivyo tu. Mtoto anajikojolea, unampiga tu mpaka aache kujikojolea. Hujui psychological issues, hujui biology, unataka kumaliza matatizo kwa shortcuts tu. Piga tu.
Ndiyo muendelezo wake huu. Una tattoo? Utapigwa tu. Maana hamna jinsi.
Hatujui kuwa hapo tunatupa talent kwa judgement ya jumlajumla.
Tukiongelea maendeleo ni rahisi sana kuongelea miundombinu, barabara, madini, mazao.
Lakini hatuongelei human capital and development of potential. Kimsingi Africa maisha ya mtu hayana thamani. Very disposable.
Ndiyo maana unaweza kuona mtu mwenye tattoo atupwe tu, si ana tattoo?
Wenzako wanasema "this is a neurodivergent talent, a creative type maybe? Let's look to see where he will fit". Wanamtafutia sehemu ataenda kufit hata kama ana mtindio wa ubongo.
Mimi miaka ya mwanzo kabisa kufika Marekani nilishangaa, nilikutana na jamaa ana mtindio wa ubongo, hata kusema anasema kwa shida. Lakini anafanya kazi supermarket anapanga maboksi. Na jamii yake inampenda. Kwenye basi kila siku asubuhi watu walikuwa wanapenda stories zake.
Jamaa akawa kama star fulani kila siku asubuhi kwenye basi tukienda kazini.
Nikasema huyu angekuwa Bongo angefungiwa ndani na familia na kuitwa ndondocha.
Wenzetu wanajua kutumia mpaka watu wenye mtindio wa ubongo. Wanawapa kazi zinazowafaa, watu wanakuwa na dignity.
Sisi ukiwa na tattoo tu, unatupwa. Hufai.
Hakuna chochote ninachotaka zaidi ya kufanya uchambuzi, mnaweza kujiamulia vyovyote mnavyotaka kuishi mkaishi hivyo. Mna uhuru huo.
Na kadiri mambo yanavyokwenda kidunia, mtakubali tu kwenda na dunia ya ushindani wa mambo ya msingi.
Either that, au mtabaki kwenye umasikini wa kudumu.
Vijananwenu wenye vipaji wataona hii nchi inaendekeza ujinga, myawasomesha halafu watawakimbia waende kufanya kazi nje.
Ujinga wa exlusivity kama hizi ndio unafanya vizazi vya vijana wa Afrika wapande viboti na kukimbilia Ulaya kutafuta maisha. Wanajiona watengwa nyumbani kwao, bila sababu za msingi.
Halafu mtabaki mnajiuliza. Mbona Watanzania wanashindwa ku perform wakiwa Tanzania, lakini wakienda nje baadhi yao wana perform sana.
Kumbe sababu zinaanzia kwenye upuuzi huu wa kuwa na stupid exclusivity.
Mtu snataka kuingia jeshini ajitolee hata kuuawa ili alinde nchi yaje, halafu unamkatalia kwa sababu ana tattoo?
Ujinga mtupu.