Mbona unarudia kile nilichokisema, hao wenye tattoo wana sekta zao, we mwenyewe umehusisha tattoo na creativity na ndiko waliko huko, wasanii, wachoraji, wahunzi wengi ndo huchora tattoo.
Halafu unaitolea mfano US wakati kule mwanzo pia uliandika nayo ina hilo tatizo.
Tungeona viongozi wa huko ulaya wana tattoo mwili mzima, wananyoa kama wasanii wa nchi hizo, ni marasta man, wanavaa t-shirt na jeans halafu wanatinga kwenye vikao vya umoja wa mataifa hapo ningeamini usemalo kua muonekano wa mtu huko ulaya hutizamwa tofauti kabisa na huku Africa.
Bado nakusisitizia kua hao wenye tattoo na wenye mionekano ifafanayo na hiyo hata iwe wapi wana sekta zao wanazofit, hata kama una ushawishi mzuri lakini unavaa kihuni watu hawatakuelewa.
Mfano waziri mkuu wa ujerumani ni shoga, rapper Lil Nas X nae ni shoga, vipi mionekano yao inafanana??
Mmoja msanii mwingine ni waziri mkuu. Kazi tofauti, mionekano tofauti lakini wapo jamii moja. Unadhani ni kwanini waziri mkuu huyo havai kama Nas??
Mfano mwingine, BBC, DW, Aljazeera ni vyombo vikubwa vya habari duniani vipi muonekano wa wanahabari wa ukoje?? Wanavaa kama wanahabari za udaku?? Kuna miiko ya muonekano kwa kila sekta.
kila sekta ina miiko yake kaka jeshini pia ni hivyo, halafu sio tattoo pekee hata makovu hayatakiwi.