Vijana wazuiwa kujiunga na Shirika la Serikali kwa kuwa na Tattoo

ULitaka mtumishi wa umma mhuni? Alilazimishwa kujichorea hiyo tatoo? Avune alichopanda
 
Hiyo kusema wenye tatto wana sectir yao ni mwanzo wa kutambua neurodivergent talent katika jamii inayoona kuwa mwenye tattoo hafai kwa chochote ni muhuni mvuta madawa ya kulevya tu.

Eventually ukifuatia falsafa ya inclusivity, falsafa ya kuwa result oriented, utakubali mwenye tattoo anaweza kuwa hata rais.

Mkuu,

Ushaona ma tattoo ya Mfalme wa Tahiland?

 
Mkuu,

Huelewi falsafa ya inclusivity ilivyofanya nchi ziendelee na exclusivity ikivyofanya nchi ziwe masikini.
 
Hayo ya uhuni umeyasema wewe ila mi sijamaanisha ni wahuni. Kwani usanii ni uhuni? Uhunzi ni uhuni? Uchoraji ni uhuni? Usuo ni uhuni?

Ujue hiyo pia ni njia ya wao kujitambulisha wanafanya nini pindi umuonapo kwa mara ya kwanza.

Kuna watu huwachukulia rasta men kama ni wahuni, wavuta bangi na tabia mbovu, lakini mimi nimeishi nao na wapo wasiofanya hivyo vyote.

Hakuna uhusiano wa tattoo na uhuni ila kila jamii ina tafsiri yake juu ya tattoo.
Ndio maana ya kua wana sekta yao.
Kule mwanzo nilikuambia muonekano wako ni moja ya nyanja ya mawasiliano kwa jamii yoyote ile.
 
Mkuu,

Huelewi falsafa ya inclusivity ilivyofanya nchi ziendelee na exclusivity ikivyofanya nchi ziwe masikini.
Sidhani kama tutafikia muafaka mkuu, ila binafsi siamini katika hilo.

Nchi zetu zina makandokando kibao yanayofanya tusipige hatua.

Kama Tz ina watu wangapi nje ya nchi?? Ni wangapi wanaondoka kwa sababu hii ??

Wewe uliondoka nchini kwa sababu gani??
 
Mkuu,

Kwani tafsiri ya jamii haitakiwi kubadilika na muda?

Yani kama jamii ikianza kwa kuona wanawake wanaovaa suruali wanakosea sana, iendelee kufikiri hivyo tu hata ikionekana mwanamke kuvaa suruali si jambo la ajabu?

Huoni kwamba hili suala la tattoo ni sawa na mwanamke kuvaa suruali tu, with time litakuwa la kawaida tu?
 
Hatuwezi kufikia muafaka kwa sababu tuna tofauti za kifalsafa.

Mimi nipo result oriented. Sijali mtu anaonekanaje as long as anafanya kazi vizuri na ana maadili ya kazi.

Ukiogopa mfanyakazi muadilifu ambaye ana overperform kwa sababu ana tattoo, hilo ni tatizo lako.

Mimi niko very inclusive.

Wewe unaona tattoo ni kikwazo. Bila hata kujali utendaji wa mtu.

Uko radhi umuajiri mtu asiyejua kazi ambaye hana tattoo na kumuacha mtu anayejua kazi mwenye tatto.

You are superficial and exclusive.
 
Yaah jamii inabadilika kila uchwao.

Labda niwe muwazi kidogo, binafsi sioni ubaya wa kua na tattoo.
Ila sasa kwa wakati huu tattoo inatafsiriwa tofauti na jamii nyingi.
Ndio maana baadhi ya sekta hawataki uwe nazo kabisa.

Kila siku mambo mapya yanaibuka, kuna uwezekano zisikubalike kabisa au zikakubalika, yote yanawezekana.
 
Aisee sasa mbona unanisemea??

Na ni kazi zipi hizo??

Nimekupa mifano kibao hapo, na wapi mimi nimeandika siwezi kumuajiri mtu kisa ana tattoo??
Wapi nimeandika niko radhi kumuajiri asiejua kazi kisa hana tattoo??

Halafu swali kuu ni hiyo kazi ni kazi gani?? Sio kila kazi zinamfaa aliechora tattoo.
 
Mbona kama unafraid double Standard hapa kuwa mvaa kata-K anajua na asiyevaa hajui kazi....Pont na hoja ni wote wawili wanajua Designing alafu mmoja ana Tattoo na mmoja hana wepi anafaa huo ndio uwiano.
 
Kuchora Tattoo sio mbaya mwili ni wako ila mbaya pale ambapo unakataliwa sehwmu fulani kama ajira kisa una tattoo then unalalamika kwanini ukataliwe wewe tatizo lipo kwako.

Kichora matattoo, rasta na lifestyle zinazoendana na hizo hakikisha wewe umejipata kimaisha na utegemei kuajiriwa sehemu kama Diamond yule, MO nk ila Jobseeker then unajichora tattoo wewe huna akili
 
Unafosi DOUBLE STANDARD jamaa
 
Kuna mambo mawili ambayo kama hatutakuwa waangalifu, tunaweza tusielewane bila sababu. Yani tunaweza juwa tunasema kitu kimoja, halafu tunabishana kwa kukisa juelewa nuktadha wa mazungumzo yetu tu.

1. Kuna kuizungumzia jamii kama ilivyo. The Actual.

Kusema mambo yalivyo. Hapa ukisema kwamba jamii yetu haifagilii tattoo na mtu reasonable anatakiwa aelewe hilo, na kujipiga tattoo katika jamii hii halafu ukategemea jamii ikuelewe na kukukubali katika kazi za serikali na nyingine kama hizo, utakuwa unakosea na huwi reasonabke, hapo nakuelewa kabisa, sina tofauti na wewe.

2. Kuna kusema jamii inavyotakiwa kuwa. Hii ni abstract thinking.

Jamii ipo hivi, ina judge sana tattoo, lakini je, hilo ni sawa? Hatuwezi kujenga jamii inayojikita katika kuangalia vitu vya ndani, vya msingi, kuwa result oriented na kuacha superficials za kuangalia nje mtu yukoje?

Hii 2 ndipo mara nyimgi nafanyia argument mimi.

Na mara nyingi napata tatizo kueleweka kwa sababu watu wengi wako stuck kwenye 1, hawawezi mazungumzo yaliyopita 1 na kwenda 2.

Mimi nikiongelea 2 wao wanarudi kwenye 1.
 
Nimemfatilia kidogo huyo mfalme, ni wazi kua hukutakiwa kumuweka hapa kama refference yako coz anazidi kudhalilisha watu wenye tattoo.
 
Kama kuchora tattoo si kitu kibaya, sasa kwa nini unakataliwa ajira kwa juchora tattoo?

Huoni kwamba this is just an arbitrary cultural construct?
 
Nimemfatilia kidogo huyo mfalme, ni wazi kua hukutakiwa kumuweka hapa kama refference yako coz anazidi kudhalilisha watu wenye tattoo.
Sikumuweka yeye kama mtu binafsi, nimemuweka kama mfano kwamba mtu mwenye tattoo anaweza hata kuwa mfalme wa nchi.

Kukataa tattoo ni arbitrary cultural construct tu.

In fact kuna Wamakonde wanaweka tattoo kiutamaduni ukiwakatalia kazi kwa sababu ya tattoo zao unawavunjia haki zao za kibinadamu za kufuata utamaduni wao bila kubaguliwa sehemu za ajira.
 
Halafu unakuta jitu jeusi kama mimi hapa nalo linachora tattoo! Pumbavu kabisa!
 
Namba moja tuko pamoja kabisa.

Namba mbili ni ngumu kuelewana na watu kwasababu ya mitazamo tofauti na ndio jamii hiyo ilivyo.

Hata mimi nlitamani sana watu wasiijudge vibaya bangi ili vijana wasiitumie vibaya, ila jamii ishaamini bangi ni mbaya, inaleta uchizi, ukiitumia unakua mwizi, kibaka, jambazi nk ila sio kweli.

Vivyo hivyo kwa tattoo jamii ya hapa kwetu inaamini tattoo ni uhuni, kuibadili hiyo ifanyike kazi.
 
Kwenye hilo tuko pamoja, sasa tumeelewana.

Hata mimi najua tattoo sio mtu.
 
Ni ujinga tu, hz sheria zingine hazina maana Sana, Wana jeshi wa USA, wengi wana tattoos, yapo majeshi wanafuga hata ndevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…