Vijana wengi hawendelei kwa sababu ya kuifuatilia vitu vichovu vinyonge na vilivyofelifeli

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Unachokifuatilia muda mrefu ndicho kinajenga ufahamu na mipaka yako kiakilini.

Acha kufuatilia mambo madogomadogo, mambo ya manenomaneno yasiyo na vitendo. Unanyong'onyesha Ubongo wako.

Mfano;
Jamaa kapata milioni 300 lakini anafikiria kwenda kufungua mpesa au kufuga tung'ombe kwenye robo heka. Hii ni KWA sababu akili imefinywa licha ya KUWA na fedha maana wakati anafanya kazi muda mwingi alikuwa anafuatilia mademu, vyakula, mipira,umbea, kutaka wamuone anazo etc.

Wakati Bado huna KITU fuatilia mambo makubwa na namna yanavyofanikishwa.

Mfano, kufuga kuku milioni moja kama wanavyofanya china huko. Nakuhakikishia huwezi kushindwa kuku 500.

Jinsi watu wanavyomanage mashamba ya Hekari 100,000 au angalau kuanzia 20000 Hekari.
Huwezi kushindwa au kuleta tmafanikio kwenye Hekari 100.

Angalia Megaprojects and engineering projects. Wanavyoanza kuanzia kwenye concept. Mbinu njia na tahadhari na uthubutu wao huwezi kushindwa kuendesha kiwanda cha mafuta ya alizeti

Angalia namna makampuni makubwa yanavyokopa mikopo ya mabilioni na kujiingizia faida ya billions. Huwezi kushindwa kumanage mkopo wa millioni mia.

Haya ndio yanapaswa kujaa kwenye akili ya mtafutaji kijana.

Ni hayo tu

Mtumishi
Matunduizi
 
Unachokifuatilia muda mrefu ndio kinajenga ufahamu na mikapa yako kiakili.

Acha kuifuatiliaambo madogomadogo, mambo ya manenomaneno yasiyo na vitendo. Unanyong'onyesha Ubongo wako.

Mfano;
Jamaa kapata milioni 300 lakini anafikiria kwenda kufungua mpesa au kufuga tung'ombe kwenye robo heka. Hii ni KWA sababu akili imefinywa licha ya KUWA na fedha maana wakati anafanya kazi muda mwingi alikuwa anafuatilia mademu, vyakula, umbea, kutaka wamuone anazo etc.

Wakati Bado huna KITU fuatilia mambo makubwa na namna yanavyofanikishwa.

Mfano, kufuga kuku milioni moja kama wanavyofanya china huko. Nakuhakikishia huwezi kushindwa kuku 500.

Jinsi watu wanavyomanage mashamba ya Hekari laki kuanzia 20000 Hekari.
Huwezi kushindwa au kuleta uzbe kwenye Hekari 100.

Angalia Megaprojects and engineering projects. Wanavyoanza kuanzia kwenye concept.

tupe kwanza mfano wako wewe unafanya mega project zipi

au ndiyo yale mambo ya motivesheno spika

za kuambiwa changanya na zako!
 
Unachokifuatilia muda mrefu ndio kinajenga ufahamu na mikapa yako kiakili.

Acha kuifuatiliaambo madogomadogo, mambo ya manenomaneno yasiyo na vitendo. Unanyong'onyesha Ubongo wako.

Mfano;
Jamaa kapata milioni 300 lakini anafikiria kwenda kufungua mpesa au kufuga tung'ombe kwenye robo heka. Hii ni KWA sababu akili imefinywa licha ya KUWA na fedha maana wakati anafanya kazi muda mwingi alikuwa anafuatilia mademu, vyakula, umbea, kutaka wamuone anazo etc.

Wakati Bado huna KITU fuatilia mambo makubwa na namna yanavyofanikishwa.

Mfano, kufuga kuku milioni moja kama wanavyofanya china huko. Nakuhakikishia huwezi kushindwa kuku 500.

Jinsi watu wanavyomanage mashamba ya Hekari laki kuanzia 20000 Hekari.
Huwezi kushindwa au kuleta uzbe kwenye Hekari 100.

Angalia Megaprojects and engineering projects. Wanavyoanza kuanzia kwenye concept.

Angalia namna makampuni makubwa yanavyokopa mikopo ya mabilioni na kujiingizia faida ya billions. Huwezi kushindwa kumanage mkopo wa millioni mia.

Haya ndio yanapaswa kujaa kwenye akili ya mtafutaji kijana.

Ni hayo tu

Mtumishi
Matunduizi
Wewe umeendelea? Kama kuandika tu huwezi......!!!???
 
uko sahihi kabisa vijana hatuna maono ya mbali..... nina ndugu yangu kipindi runajitafuta hatuna hili wala lile nikawa namwambia mm nikifanikiwa kupata sehemu nikawa naingiza hela kidogo nitajitahidi niwekeze kwenye mifugo kwake ilikua ngumu kunielewa ikawa tukipiga stori za kuhamasishana yeye anaweka changamoto zionekane nyingi zaidi ya mafanikio..... siku moja niliamua likizo ya kazini nikiwa home nikatembee kwa wamasai kutafuta kujuana nao kwa bahati nikakutana na dada tulisoma naye basi ikawa heri sana akanitambulisha kwao na nikaeleza nia yangu ya kutamani ufugaji..... nilipoondoka pale lengo likawa limeanza kuota mizizi siku zinavyokwenda naboresha mawasiliano naye na mzee wake.......
nikapataga kahela ka kuokota basi nikaweka kondoo 6 na mitamba miwili kwake tena kwa imani tu nikasema moyoni nikipigwa basi japo watu wanafanya hivyo sikua mchoyo maswala ya dawa za muhimu na jamaa yangu akawa ananipa kauli za kukatisha tamaa mara wamasai watakutapeli ila cha ajabu zile ng'ombe zilipo zaa tu nikaitwa nikaweke alama mifugo yangu tukaemdelea hivyo mpka nikaamua kutenga kundi langu nikaomba na kijana wake achunge na yeye aanzishe kundi lake pale pale kwenye zangu yote haya niliweza kuyajua kupitia mawasiliano na kuamua kulivaa jambo leo si haba sinunui nyama siku za sherehe na hao hao ndugu jamaa na marafiki nawauzia kulingana na uhitaji wao.... ndugu yangu mpaka leo haelewi nini nafanya na siku zote huniona niko vile vile kwakua anasubiri aone ndipo aamini....
 
Na sisi above 50, Tufanyeje?!
 
kwa mfano huyo kijana aliepata hela ndefu kama hiyo,huwezi kumwambia kitu wakati akiwa viwanja,ataaendelea hivyo hivyo mpaka zikibaki kama milioni kumi ndio ataanza kuomba ushauri afanyeje na hiyo hela,sana sana itaisha tu maana hela inayokuja bila mipango huisha tu.
 
uko sahihi kabisa vijana hatuna maono ya mbali..... nina ndugu yangu kipindi runajitafuta hatuna hili wala lile nikawa namwambia mm nikifanikiwa kupata sehemu nikawa naingiza hela kidogo nitajitahidi niwekeze kwenye mifugo kwake ilikua ngumu kunielewa ikawa tukipiga stori za kuhamasishana yeye anaweka changamoto zionekane nyingi zaidi ya mafanikio..... siku moja niliamua likizo ya kazini nikiwa home nikatembee kwa wamasai kutafuta kujuana nao kwa bahati nikakutana na dada tulisoma naye basi ikawa heri sana akanitambulisha kwao na nikaeleza nia yangu ya kutamani ufugaji..... nilipoondoka pale lengo likawa limeanza kuota mizizi siku zinavyokwenda naboresha mawasiliano naye na mzee wake.......
nikapataga kahela ka kuokota basi nikaweka kondoo 6 na mitamba miwili kwake tena kwa imani tu nikasema moyoni nikipigwa basi japo watu wanafanya hivyo sikua mchoyo maswala ya dawa za muhimu na jamaa yangu akawa ananipa kauli za kukatisha tamaa mara wamasai watakutapeli ila cha ajabu zile ng'ombe zilipo zaa tu nikaitwa nikaweke alama mifugo yangu tukaemdelea hivyo mpka nikaamua kutenga kundi langu nikaomba na kijana wake achunge na yeye aanzishe kundi lake pale pale kwenye zangu yote haya niliweza kuyajua kupitia mawasiliano na kuamua kulivaa jambo leo si haba sinunui nyama siku za sherehe na hao hao ndugu jamaa na marafiki nawauzia kulingana na uhitaji wao.... ndugu yangu mpaka leo haelewi nini nafanya na siku zote huniona niko vile vile kwakua anasubiri aone ndipo aamini....
Hii naichukua kama ilivyo naifanyia kazi 👏
 
amini mkuu hutafeli kwa wamasai au wafugaji zingatia mawasiliano na usiwe bahili wa vitu vidogo kama dawa ndugu hutajuta ila msingi mkubwa wafanye wawe watu wako wa karibu
 
Back
Top Bottom