Vijana wengi wa kitanzania hawajui namna ya kuzika wapendwa wao

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Vijana wengi hasa wa mijini hawajui ni namna gani ya kuwazika wapendwa wao, hii nimeiona kwenye misiba kadhaa hasa ya kikristo wazikaji wanakodiwa.

Kwanza ni waoga kuingia mortuary hawawezi kabisa, wakati wa mazishi kuingia kaburini wengi wao hawawezi kabisa kazi kunyoa viduku na kuvaa suruali nusu makali.

Unakuta mtu kafiwa na baba yake mzazi anaambiwa ingia umzike baba yako anabaki amekodoa mimacho tu hajui aanzie wapi.

Vijana wa vijijini wapo vizuri wanajua kutekeleza haya majukumu ila mijini ni sifuri.
 
Sio wote unazungumzia wa kishuwa mkuu, uswahilini uyo mpendwa wako anazikwa na jamaa zake labda upate wasaa wakwenda kumwandaa montuq
 
Kwa wakristu naona hamna shida sana labda kwa waislam maana wana utaratibu maalum kuanzia kuosha mpk kuzika.
 
Vijana wengi hasa wa mijini hawajui ni namna gani ya kuwazika wapendwa wao, hii nimeiona kwenye misiba kadhaa hasa ya kikristo wazikaji wanakodiwa.

Kwanza ni waoga kuingia mortuary hawawezi kabisa, wakati wa mazishi kuingia kaburini wengi wao hawawezi kabisa kazi kunyoa viduku na kuvaa suruali nusu makali.

Unakuta mtu kafiwa na baba yake mzazi anaambiwa ingia umzike baba yako anabaki amekodoa mimacho tu hajui aanzie wapi.

Vijana wa vijijini wapo vizuri wanajua kutekeleza haya majukumu ila mijini ni sifuri.
Ungeweka mwongozo na source yake
 
Back
Top Bottom