Si kweli, kuna watu wanatoka Mali, Cameroon, Nigeria etc. wanakwenda kuzamia USA wakiwa na hizo hizo lugha gongana. Moja ya sababu kubwa inayofanya wabongo wasizamie sana nchi za ng'ambo ni utulivu wa kisiasa hali ya uchumi/maisha inayo stahimilika pia ujamaa wetu umetufanya kwa namna fulani kuwiana ki maisha na fursa pia, mfano leo hii mTanzania anaweza kutoka singida akafika DSM akaanza kuzungusha CV ofisi mbali mbali ama kuomba hata kupiga kazi za vibarua na asiulizwe hata kabila ama dini yake, ila nenda hapo Kwa jirani zetu Kenya huwezi/ni ngumu sana kupata kazi/kibarua kama kabila lako si la mwenye kampuni ama bosi wa eneo husika, pia hata ukikutana na mtu katika kufahamiana tu akikuuliza unaitwa nani atataka asikie jina la ukoo wako ili aweze ku tune mazungumzo yake.
Kwenye utulivu wa hali ya ki siasa na usalama tazama nchi kama Nigeria ama zingine za huko west, watu hawana amani wala uhakikawa usalama wa maisha yao, Serikali zinaongozwa na familia chache huku asilimia kubwa ya wananchi wakiwa kwenye lindi la umasikini, katika hali kama hiyo raia wako tayari kuhatarisha maisha yao kwa kutumia hata njia ngumu kufika nchi za ulaya ili kuyatafuta maisha bora.