Vijana wengi wanaokimbilia mijini wakitokea vijijini wanajiandaa kuzeeka wakiwa maskini

Vijana wengi wanaokimbilia mijini wakitokea vijijini wanajiandaa kuzeeka wakiwa maskini

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!
Kasi ya vijana kukimbilia mjini hasa Dar es Salaam imekuwa kubwa mno na inatisha. Ni kawaida sasa kila kijana uliyesoma naye primary au sekondari ukimuulizia yuko wapi atakuambia yuko Dar.

Ilinifanya mpaka Takwimu za NBS kuhusu idadi ya wakazi wa Dar es Salaam niliona imepunguza idadi. Hawa vijana wanafanya kazi za nguvu ili kujipatia ridhki ya kula leo na kesho tu. Wengine wanaishi kwa umachinga na wachache wameajiriwa.

Miaka 30 mbele tayari wengi watatupwa nje katika shughuli zao naturally. Na hapo wazee maskini na ombaomba wataongezeka.
 
Kijijini hakuna maisha kama ya mjini. Wacha waje wapambane, umaskini wa mjini na umaskini wa Kijijini ni umaskini wa aina 2 tofauti.
 
Kitu nimejifunza hakuna anayejua chochote kuhusu maisha. Wengi tunaongelea nadharia za kufikirika kuhuisha na uzoefu. Unapaswa kuelewa hata wewe kuna mahali unakwama na kila mtu anapitia changamoto zake. Kama huna suluhisho acha watu wapambane.
 
Kweli aisee mimeenda kijijini sikumkuta hata mmoja ambae nimesoma nae wote wapo Dar.
 
Kijijin hakun maisha kama ya mjini. Wacha waje wapambane, umaskin wa mjin na umaskin wa Kijijin ni umaskin wa Aina 2 tofaut
Vijana wengi waliofanikiwa zaidi jiji hili ni wale walioingia na mitaji ya kufanya na waajiriwa hawa machinga wanaokuja bila chochote asilimia kubwa hali ni tete kitu kingine kununua ardhi kwa mkoa huu ni ngumu gharama za maisha zipo juu Sana kuanzia usafiri umeme na chakula hivi vitu vinakost Sana jiji hili.
 
Kwamba umeme wa Dar ni tofauti na wa mkoani ki gharama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom