Vijana wengine waibukia hospitalini Dodoma kutaka kuuza figo

Vijana wengine waibukia hospitalini Dodoma kutaka kuuza figo

Hii umekaa vipi tena!? Yaani unachukua figo toka kwa mtoto wako,wewe umeishi miaka mingi unataka mtoto aishi kwa kuunga unga,kwangu Mimi naona kama hii haijatulia na Mimi siwezi ukubali mtoto wangu atolewe figo kwa akili yangu!!
 
Hawezi kiri hadharani italeta mtafuruku kwenye jamii,,,lakini other side biashara inaendelea kama kawa!!!
 
Hii kitu italeta madhara makubwa sana huko mbele kama mauwaji ya watu wasio na hatia na human traficking nyie ipigieni debe muone km ni sifa Tena na ndo hvyo nchi imefunguka we shall see
 
Wakiruhusu figo zitanyofolewa sana na mauaji yatakuwa mengi

Wafanye mtu akifa viungo vyake ni vizima vihifadhiwe na kupewa wagonjwa ila iwe hiari kwa mgonjwa

Hawakutangazii, naamini wanauliza ndugu watu wakikaribia kufa
 
Mm nafikiri serikali iendelee kukataa kuuza vioungo
Lkn wachukue toka katika ajali mbali mbali zinazotokea nchini maana vile viungo vinapotea bure.
Bila kusahau kuwapa elimu wanachii juu ya faida na hasara ya biashara ya viungo.
 
View attachment 2549000
Siku chache baada ya uongozi wa Hospitali ya Bugando Mwanza kuelezea kadhia wanayoipata kutokana na vijana kuulizia iwapo wananunua figo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa Dk Alphonce Chandika naye leo Jumatatu Machi 13, 203 ameeleza kuwepo na wimbi la vijana wanaopiga simu hospitalini hapo kuuliza ikiwa wanaweza kuuza figo zao.

Dk Chandika amesema hadi sasa amepokea simu zisizopungua nne kutoka kwa vijana hao wakidai kutaka kuuza figo hali aliyoieleza kuwa ni kutokana na changamoto za maisha.

"Hili suala lipo unakuta vijana maisha yana changamoto halafu anajua Benjamin Mkapa wanapandikiza figo, wamekuwa wakipiga simu. Niwaombe huo utaratibu haupo na sheria zetu haziruhusu biashara ya uuzaji wa viungo na hata tukigundua kuna biashara imefanyika tunasitisha mara moja," alisema Chandika.

Dk Chandika ameyasema hayo leo Machi 13, 2023 wakati akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya huduma ya upandikizaji figo iliyoanza kutolewa hospitalini hapo mwaka 2018.

Aidha Chandika amesema katika kipindi hicho wamekutana na changamoto ya ukosefu wa elimu kwa baadhi ya ndugu na kushindwa kutoa figo wakihofia kufariki dunia.

Akizungumzia huduma hiyo Faraji Shabani aliyepandikizwa figo aliyopewa na mtoto wake amesema huduma hiyo imesaidia kuokoa maisha yake kutokana na kuugua muda mrefu.

Aidha Shabani amewaasa wananchi kujiunga na huduma ya Bima ya Afya kwa Wote kwani baadhi ya huduma katika upandikizaji wa figo hufidiwa kwa mgonjwa mwenye bima.

Naye Neema Sweti aliyempa figo kaka yake alisema alipata ujasiri huo baada ya kupata semina ya huduma hiyo mara kwa mara na sasa anaendelea vizuri baada ya miaka mitano tangu atoe figo yake.

MWANANCHI
Kama Kuna Mtu ana mgonjwa naweza msaidia Figo life is about donation and not Duration natamani kufanya kitu Kama hicho kuokoa maisha ya Mtu hapa Duniani .
 
Back
Top Bottom