Vijana wenzangu msipoteze muda wenu kusubiri hela za Google, Facebook na TikTok kwasababu ni hela za chai, mtachelewa kufanikiwa

Vijana wenzangu msipoteze muda wenu kusubiri hela za Google, Facebook na TikTok kwasababu ni hela za chai, mtachelewa kufanikiwa

Mfano una App yako inapata watumiaji 300k tu kwa mwezi? ukiweka admob unakua na uhakika wa dola 100 kwa mwezi...Sasa sijakwambia ukiwa na user 1M tu Trust me unaweza kujenga kwa pesa za Admob
Du! Watumiaji 300k dollar 100 kwa mwezi si kazi ya kanisa hii au umekosea hesabu zako mana kuwapata hao watumiaji 300k ni mziki
 
Vijana wenzangu, maendeleo makubwa mnayoyaona hapa Tanzania ikiwemo biashara kubwa, majumba makubwa na magari ya kifahari hayajapatikana kwa hela za mitandaoni

Bali maendeleo haya yalipatikana kwa kufanya kazi kwa bidii kubwa ndipo mafanikio haya yakapatikana

Nyumba mnazoziona Salasala, Mbezi Beach, Masaki, Goba na kwingineko zimepatikana kwa juhudi kubwa ya kazi zinazoeleweka kama biashara kubwa, ajira kubwa Serikalini nakadhalika na sio kupitia hela za mitandaoni

Hivyo basi msipoteze muda wenu mitandaoni bali muamini kwenye kufanya kazi za kueleweka sio hivyo tu bali juhudi na nidhamu ya pesa inahitajika
Hii pesa at kwa mshahara huifikishi ni njia ya mtandao tu
 
Ningesema pesa ilipo mtandaoni sema labda wewe ni serikali unataka uanzishe makato na tozo
 
Back
Top Bottom