Vijana wetu 10 waliokuwa kwenye mafunzo ya JWTZ wamepoteza maisha

Vijana wetu 10 waliokuwa kwenye mafunzo ya JWTZ wamepoteza maisha

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wakuu,

Unajua haya mambo ya Jeshi sijui inakuaje kama mtu ukifiwa. Juzi tumepata msiba wa Vijana wetu zaidi ya kumi walikuwa kwenye Mazoezi. Leo ndo tunaaga hapa Lugalo Dar, kwa anayetaka kushiriki mazishi aje.

Naamini Jeshi litatolea ufafanuzi taarifa hii ili kuondoa sintofahamu.

Baada ya hapa tunaenda Muguani.

Rais Magufuli katika hotuba yake baada ya anaapisha, ameligusia hili swala la vifo kwa uchache. Naamin leo Msemaji wa JWTZ atatupatia majina na chanzo cha vifo hivi kwa siku moja.
Narudia tena kutoa pole kwa misiba iliyotuandamana kwa hivi karibuni kwa ndugu zetu 20 wa Moshi, kule Lindi zaidi ya watu 21 na sehemu zingine waliopatwa na mafuriko na ajali mbalimbali. Pia, tuna vijana wetu 10 walikuwa kwenye mazoezi ya JWTZ nao walifariki.
Kasema Rais Magufuli.

Mungu aziweke Mahali Pema Peponi

Vijana wetu.

Majina ya waliofariki
2295107_IMG_20200203_163532.jpg


======

Wanajeshi 10 wa Tanzania wapoteza maisha wakati wakifanya mazoezi

Feb 03, 2020 14:09 UTC

Jeshi la Ulinzi la Tanzania limetangaza kuwa askari 10 wa jeshi hilo wamepoteza maisha wakati wakifanya mazoezi.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ambapo ameongeza kuwa sampuli za wanajeshi hao waliopoteza maisha katika mazoezi ya kijeshi zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi. Mabeyo ameyasema hayo leo katika ikulu ya Dar es Salaam baada ya Rais John Pombe Magufuli kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hapo Januari 31, 2020. Kwa mujibu wa Mabeyo, wanajeshi hao walikuwa kwenye mazoezi ya kawaida ya kutembea. Ameendelea kubainisha kuwa baada ya saa mbili hali zao kuanza kubadilika wakiwa eneo la Msata, walipelekwa hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ameendelea kufafanua kuwa baada ya kulazwa hospitalini hapo, baadhi yao walifariki dunia na wengine hali zao ziliimarika na kwamba hadi sasa kuna majeruhi watano. Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alitoa pole kutokana na vifo vya watu 20 katika kongamano la mhubiri wa Kikristo, Boniface Mwamposa vilivyotokea mjini Moshi, vifo vya watu 21 mkoani Lindi baada ya nyumba zao kusombwa na maji na vifo vya wanajeshi hao 10. "Tunahisi walikula chakula chenye sumu, labda wakati wanatembea walinunua vyakula barabarani vikawadhuru. Mazoezi yalikuwa ya kawaida tu. Tumepeleka sampuli za waliofariki kwa Mkemia Mkuu ili kubaini chanzo hasa cha vifo," amesema Mabeyo akizungumzia vifo hivyo vilivyotokea Januari 30, 2020.
View attachment 1346365



Sent using Jamii Forums mobile app

UPDATES;
1. Vijana 10 wa JKT Msata kufariki wakiwa kambini wa kuwajibika wawajibike tu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amesema sampuli za wanajeshi kumi waliokufa katika mazoezi ya kijeshi kwenye kambi ya Kihangaiko Mkoani Pwani zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi.
 
May be ilikuwa ajali tu.

Hata mafunzo ya kikomando hawawezi kufa askari wanafunzi 10 kwa mkupuo. Tatizo maaaskari wa vyeo vya chini wanapoachiwa kusimamia vijana wanawapa mafunzo na kazi ambazo haziko kwenye ratiba ya mafunzo.

Mti unakatwa anatokea kichaa mmoja anawaambia madogo waudake, mto una maji mengi anatokea kichaa mmoja anawalazimisha vijana waingie kuogelea huku wengine tangu wazaliwe hawajawahi kuugusa hata mfereji.

Hapa ndipo Ajali huweza kutokea.
 
May be ilikuwa ajali tu.
Hata mafunzo ya kikomando hawawezi kufa askari wanafunzi 10 kwa mkupuo.
Tatizo maaaskari wa vyeo vya chini wanapoachiwa kusimamia vijana wanawapa mafunzo na kazi ambazo haziko kwenye ratiba ya mafunzo.
Mti unakatwa anatokea kichaa mmoja anawaambia madogo waudake, mto una maji mengi anatokea kichaa mmoja anawalazimisha vijana waingie kuogelea huku wengine tangu wazaliwe hawajawahi kuugusa hata mfereji.
Hapa ndipo Ajali huweza kutokea
'Mti unakatwa anatokea kichaa mmoja anawaambia madogo waudake'

No wonder jamaa hua wanawaita wenzao(police) ni raia wakakamavu.

dodge
 
Back
Top Bottom