Vijana wetu 10 waliokuwa kwenye mafunzo ya JWTZ wamepoteza maisha

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wakuu,

Unajua haya mambo ya Jeshi sijui inakuaje kama mtu ukifiwa. Juzi tumepata msiba wa Vijana wetu zaidi ya kumi walikuwa kwenye Mazoezi. Leo ndo tunaaga hapa Lugalo Dar, kwa anayetaka kushiriki mazishi aje.

Naamini Jeshi litatolea ufafanuzi taarifa hii ili kuondoa sintofahamu.

Baada ya hapa tunaenda Muguani.

Rais Magufuli katika hotuba yake baada ya anaapisha, ameligusia hili swala la vifo kwa uchache. Naamin leo Msemaji wa JWTZ atatupatia majina na chanzo cha vifo hivi kwa siku moja.
Kasema Rais Magufuli.

Mungu aziweke Mahali Pema Peponi

Vijana wetu.

Majina ya waliofariki


======


UPDATES;
1. Vijana 10 wa JKT Msata kufariki wakiwa kambini wa kuwajibika wawajibike tu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amesema sampuli za wanajeshi kumi waliokufa katika mazoezi ya kijeshi kwenye kambi ya Kihangaiko Mkoani Pwani zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi.
Your browser is not able to display this video.
 
May be ilikuwa ajali tu.

Hata mafunzo ya kikomando hawawezi kufa askari wanafunzi 10 kwa mkupuo. Tatizo maaaskari wa vyeo vya chini wanapoachiwa kusimamia vijana wanawapa mafunzo na kazi ambazo haziko kwenye ratiba ya mafunzo.

Mti unakatwa anatokea kichaa mmoja anawaambia madogo waudake, mto una maji mengi anatokea kichaa mmoja anawalazimisha vijana waingie kuogelea huku wengine tangu wazaliwe hawajawahi kuugusa hata mfereji.

Hapa ndipo Ajali huweza kutokea.
 
'Mti unakatwa anatokea kichaa mmoja anawaambia madogo waudake'

No wonder jamaa hua wanawaita wenzao(police) ni raia wakakamavu.

dodge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…