Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Habari wana JF.
Leo nawaletea vijiji maarufu zaidi Tanzania bara.
1. Kolomije: Hiki kipo wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Hiki kilijipatia umaarufu kuliko vijiji vyote tangu march 2017. Hiki ni kijiji alichozaliwa Mheshimiwa Paul Makonda, RC Dar.
2. Butiama: Hiki kipo wilayani Butiama mkoani Mara. Huko ndiko alikozaliwa mwasisi wa Taifa hili Julius Nyerere.
3. Msoga: Hiki kipo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Huku ndipo anapoishi na nyumbani kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
4. Lupasu: Hiki kipo wilayani Masasi mkoani Mtwara. Huku ndipo alipozaliwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
5. Ngarash: Hiki kipo wilayani Monduli mkoani Arusha. Huku ndiko alipozaliwa Edward Lowassa.
NB: Chato sio kijiji bali ni mji na halmashauri iliyopo wilayani Chato mkoani Geita.
Nawasilisha.