Vikampuni vya mikopo online ni vikundi vya kausha damu, hivi Benki kuu imevisajili kweli? Mbona Zuri pesa wanatukana hivi?

Vikampuni vya mikopo online ni vikundi vya kausha damu, hivi Benki kuu imevisajili kweli? Mbona Zuri pesa wanatukana hivi?

Sifi Leo

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
6,408
Reaction score
12,100
Aise, kwema wadauh? Leo nimecheka sana mwanangu mmoja alikopa elfu 40,000 wakampa 24,000/= badala ya 40,000 aise nilishangaa jamaa akala kiapo cha kutokulipa deni hilo, sasa hizo simu kutoka kwa zuri pesa ni balaa.

Jamaa akaamua kuwatandika block la maana weee!
UJUMBE uliofatia hapo ni balaa matusi ya nguoni kwa jamaa miksa kutukania mama yake, mara kudai jamaa anajiuza ili alipe deni ili Hali jamaa ni wa kiume.

Najiuliza hivi vikampuni vimesajiliwa na Benki kuu kweli?
Mkopo wa elfu 40,000 unariba ya 16000 kwa wiki?
Halafu mtu kapokea mkopo wa 40,000 ila amekatwa, Sasa anatakiwa alipe 40,000 so kwa wiki analipa 56000

Hii nchi ukitaka kutoboa ungana na Dola kuwaibia wananchi wa Hali ya chini ndo hii. Ila kama kweli vikampuni hivyo vimesajiliwa na serikali kupitia benki kuu!
 
Havina nguvu, wewe ukiweza kuvikopa kopa na gharama yako itakuwa kutukanwa kama hivo.

Zamani walikuwa wanatumia info zako kukudhalilisha kwenye mitandao ya kijamii, Kwa ndugu hata wafanyakazi wenzako.

Lkn benki ikawapiga biti kwani ni kinyume na maadili ya sheria ya kukopa na kuweka, hivo sahivi wanaishia kukutana tu ila hawawezi kukufanya chochote zaidi ya hapo.

Ni kama tuu wanaoiba fedha za umma adhabu yao tuwachambe tuu mpaka waone aibu.
 
Aise, kwema wadauh? Leo nmecheka sana maanangu mmoja alikopa mkopo wa elfu 40,000 wakampa 24,000/= badala ya 40,000 aise nilishangaa jamaa Akala kiapo cha kuto, kulipa deni ilo Sasa hizo simu kutoka kwa zuri pesa ni balaaa.

Jamaa akaamua kuwatandika block la maana weee!
UJUMBE uliofatia hapo ni balaaa matusi ya nguoni kwa jamaa mikisa kutukania mama yake, mara kudai jamaa anajiuza ili alipe deni ili Hali jamaa ni wa kiume.
Jamani mikisa kukwambia anauza kinyero alipe mkopo wa zuri pesa najiuliza hivi vikampuni vimesajiliwa na Benk kuu kweli?
Mkopo wa elfu 40,000 unariba ya 16000 kwa wiki?
Alafu mtu kapokea mkopo wa 40,000 ILA amekatwa 16000 Sasa anatakiwa alipe 40,000 so kwa wiki analipa 56000 hii nchi ukitaka kutoboa ungana na Dola kuwaibia wananchi wa Hali ya chini ndo hii. ILA kama kweli vikampuni hivyo vimesajiliwa na serikali kupitia benk kuu!
Nasikia hivyo vikampuni ndo matawi mama ya hizo benki
 
Mtu anawezaje kukopa 40,000 wakampa 24,000? 😁
Na yeye anapokea hiyo fedha! 😁
Hii tuu kwa mtu mwenye akili timamu mi "red flag" kwamba hapo analia.
 
"Jamaa yangu kawapiga bonge la block'' ili asilipe deni lake,ni kama vile unamsifu kwa alichokifanya,
Halafu hapo hapo unalaumu "Hii nchi ukitaka kutoboa ungana na dola kuwaibia wananchi..."

Yani hapo mwizi mmoja ambaye ni huyo jamaa yako unamsifia kisha unalaumu hao wakopeshaji!!
Wizi ni wizi tu kijana,
Tukemee wizi wa aina zote,wizi mkubwa na wizi mdogo yote ni wizi tu.
 
mimi nashauri alipe deni .. kunyume na hapo atastair adhabu .. hasa hata karma huenda ikamhusu alikopa ilipaswa kurejesha kisha asirudie .. uaminifu kwanza....basi angalau airejeshe 24 ile ile
 
Back
Top Bottom