Vikontena / vifuko vya kuwekea pesa za mauzo havitoshi ama nafasi inbaki, Naweza kupata wapi vimifuko ama container vya kimo nachohitaji

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178





Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana muajiriwa na pia ni mfanya biashara

Katika biashara yangu huwa napenda sana kuiendesha kwa kuongezea vitu vya darasani, kuna hii system nataka niitumie ya kutenganisha pesa za mauzo mfano ya kwa siku, baada ya siku kadhaa, kwa wanaolipa madeni, kulingana na wateja, n.k..

Sasa nilipata wazo ninunue vikontena na vimfuko vigumu vya plastiki nikajaribu ila napata wakati mgumu kuziingiza pesa kwa mpigo

Shida kwenye hivi vikontena na vifuko nikijaribu sana inaingia milioni 2 tu, mbaya zaidi unakuta jioni kuna milioni 3 hadi 6 kwahio inakuwa changamoto kweli kweli

Ni wapi naweza kupata contena ama vifuko vigumu kwa saizi nayaotaka mimi ili pesa ikiingia iwe inabaa vizuri na kusiwe na nafasi ya ziada, makontena ya vyakula nimejaribu ila yanaacha nafasi.
 
Jamiiforums uwanja wa watu wengi huu natumani nitapata msaada
 
Tajiri....haloo.....tajiri🤣
Faida =bei ya kujumua mzigo - (kuusafirisha + gharama za kuushusha + gharama za kuutunza stoo + mizigo inayofika imeharibika + mshahara wa mabinti wa dukani + chakula na usafiri mabinti wa dukani + TRA + Leseni ya biashara).

Faida ndogo
 
Yani huwezi kuweka hesabu kwenye notebook au computer?dunia inenda mbele ww unarudi nyuma au ni masharti ya mganga?
Kuweka kwenye note book naweka ila sasa kuzitunza pesa kama kwenye hizo notebook / excel katika mfumo wa mauzo ya siku, madeni yanayolipwa, pesa za mauzo kwa wateja wakubwa, n.k. hapo ndio inakuwa shughuli.
 
Umepewa hizo hela za shemeji yako na dada yako ufiche wewe rinda limeshaanza kulia mbwata
 
Sigawi hata shilingi 50, asiefanya kazi na asile
Kwani wamakataa kazi hata ya 3some?!

Kwa hiyo ingekuwa unaendesha Benki pesa ya kila mteja ungeweka kwa ki kontena tofauti?!

Wenzio huchanganya pesa, rekodi ya miamala ndo hutofautisha mambo.

Anyway, Lipia Tangazo
 
Yani huwezi kuweka hesabu kwenye notebook au computer?dunia inenda mbele ww unarudi nyuma au ni masharti ya mganga?
Mleta mada hana lolote, huo ni mtego tu, kuna mtu anaenda kulizwa soon kwa tamaa zake
 
Kwani wamakataa kazi hata ya 3some?!

Kwa hiyo ingekuwa unaendesha Benki pesa ya kila mteja ungeweka kwa ki kontena tofauti?!

Wenzio huchanganya pesa, rekodi ya miamala ndo hutofautisha mambo.

Anyway, Lipia Tangazo
Mimi ndiyo nimejua leo kuwa pesa inawekwa kwenye kikontena
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwamba mjanja sana atapigwa mtu soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…