Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwa Taifa la Israel mnamo 1948, serikali ya Marekani ambayo imekuwa mshirika mkuu wa siasa na harakati za Israel pale Mashariki ya Kati, imeeleza kusudio lake la kuweka vikwazo kwa kikosi maalumu cha Jeshi la IDF kilichofanya oparesheni zake upande wa ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na masettler wa Israel
Vikwazo hivyo vinahusu kikosi hiko kuwekewa vikwazo maalumu ikiwemo kutotumia fedha zozote zinazotokana na ufadhili wa Marekani.
Mimi binafsi msimamo nilionao ni kutounga mkono vita aina yeyote ile. Sababu kuu zinazonisukuma kuwa na msimamo huo ni pamoja na
Source: www.timesofisrael.com

- Athari za vita kwa maisha ya wanadamu hususan waathirika wakuu watoto na wanawake
- Athari kwa mazingira, hakuna vita inayoacha salama mazingira ambapo pamoja na uharibifu mkubwa unaoonekana, bali kemikali za silaha zinazotumika na masalia vitaendelea kuwa tishio kwa mazingira na hali ya hewa sambamba na viumbe tegemezi kwa mazingira hayo
- Mahusiano baina ya raia kati ya pande za vita kuvunjika na hatimaye kuzaliwa kwa doctrine ya chuki, kubaguana na kuviziana
- Athari za kiuchumi kwa wahusika na wasiohusika na vita hizo
Source: www.timesofisrael.com