PostGE2025 Vikwazo vya umoja wa Ulaya: CCM kuanzisha harambee kwa wafanyabiashara lengo kukusanya bilioni 100 kila mwezi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
The coming economic crisis kila mtu atalia.
Kila sekta itaathirika .
Hizo mbwembwe za michango zitakua za miezi 3 ya mwanzo baadae vilio na kusaga meno vitaenea Nchi nzima.

Hawa mashetani kama kweli ni wazalendo na wanaipenda kweli Tanzania basi solution ni ku step down for the sake of the Nation and innocent civilians.
 
Wataalumu wa uchumi wa chama cha mapinduzi wamependekeza ianzishwe harambee ili wafanyabiashara wenye mapenzi na chama watakuwa wanachanga bilioni 100 kila mwezi.
Ukute hao "wataalamu" walioshauri hivyo ni akina baba LEVO.

Ukata ukirindima ndani ya nchi wahanga wa mwanzo kabisa ni biashara, zinakufa kifo cha mende.

Jana imesemwa humu kuwa mahoteli ya Zenji yanategemea watalii na sasa hayana wateja kabisa.

Sasa subiri ipite mwezi mmoja, miwili, nk, ukaombe hizo billion kwa hao wamiliki uone kama watakupa wakati kulipa mishahara tu itakuwa ishashindikana.

Serikali itakosa pesa ya kulipa mishahara kwa polisiccm, afu hawa wataongea Lugha moja na GenZ, ndipo hapo ccm watajua hawajui chochote
 
Majinga hawajui uchumi the way unavyo fanya kazi nadhani baada ya kunyimwa pesa na EU kama wasipo wajibikia matakwa ya EU kifuatacho kiwe ni kufukuzwa Kwa mabalozi wote wa nchi zilizopo EU then TZ Ipigwe ban kuuza na kununua bidhaa katika nchi zote za EU ,


Hapo ndio itakuwa patamu sana
 
Hivi kumb2 Ccm bado ipooo? Mbona kimya sanaa Mzee wa gombe yupoo? Qale ma chawaa siwasikii kabisaa.....kulikonii???
 
Hawajui hawa wakianza kukubana wanaenda hatua kwa hatua. Leo wamefuta misaada ya kwenye bajeti, ukiendelea kuleta kiburi, wanazuia kufanya biashara na wewe. Hakuna utalii wala kupeleka bidhaa zako kwao. Baadae ukiendelea na kiburi, wanakuja kuwawekea vikwazo viongozi binafsi na familia zao pamoja na kufungia account na kukamata mali zao. Hatua kwa hatua.

Wanadhani watakimbilia China na Uarabuni ila wanajidanganya.
 
Serikali ipunguze matumizi, mikoa ipunguzwe kutoka 26 hadi 17 wilaya zipunguzwe kutoka 160+ hadi 80.

Serikali itumie magari aina ya Toyota RAV4 kwa wote wakiwemo mawaziri hadi mikoani na wilaya watumie Suzuki Vitara hata endapo hawa watawala wa sasa wataondolewa mwezi ujao lkn serikali ya mpito itakayokuja ifanye hivyo hivyo.

Posho zote zifutwe na watumishi wote wakiwemo wabunge wabaki na mishahara tu na vikao vyote vifanyike kwa Video Conference badala ya watu kusafiri kutoka wilayani kwenda mikoani au kwenda Dodoma.

Rais asicheze na fedha za umma eti kununulia magoli na fedha za ikulu zifanyiwe ukaguzi mkali kabisa na CAG kwani kuna ubadhirifu mkubwa sana huko.
 
Hayo yote ya kubana matumizi yakifanyika ndiyo yanazidisha kuanguka kwa uchumi. Waende kwenye hizo Vitara sijui ina maana kununua tena maelfu ya magari mapya, hizo ni gharama zingine. Na kwa uchumi unaoanguka hayo ma V8 watayapeleka wapi, nani atayanunua au ndiyo watayapaki hadi yaozeane?

Cha muhimu wakubaliane na hali, wamekosea. Waangalie nani wa kumtoa kafara, tusafishe nchi. Kiburi hakitawasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…