Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Wacha na mimi nitie neno hapo mkuu, Vikwazo vya kiuchumi vina mbio mbili.
i, Mbio fupi[ short run ] na
ii, Mbio ndefu[ long run ]

- Kwenye mbio fupi{ short run }, mwanzoni kabisa mwa operation ya kivita ya Urusi nchi Ukraine baada ya Vikwazo kuanza Urusi ilitaka kushindwa Ila baada ya kukaa kwa wachumi wa ndani ya Urusi na kuweka mipango bomba wakaweza kushinda mpaka Sasa mfano kutoka kushuka kwa rubble na kupanda kwake haraka Sana mwezi wa tatu na hii kutokana na rubble Kutumika Sana kwa manunuzi baada ya Bank kuu ya Urusi kuamrisha malipo yote ya ununuzi wa rasilimali kutoka Urusi ni lazima rubble itumike Kama fedha kuu ya manunuzi na hapa umoja wa ulaya uliweza kushindwa na Urusi. Mpaka Sasa tunaona Urusi bado anasimama lakini si kwamba anasimama kwa nguvu Kama awali kabla ya Operation yake ya kijeshi kuanza huko Ukraine la hasha . Ana simama sawa lakini si kwa ubora Kama wa awali.

- Kwenye mbio ndefu{ long run } hapa inahitajika akili nyingi zaidi za wachumi wa Urusi kuliko hata mbio fupi hapa ni mbio za kuweza kuishi na vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu na huku ukivishinda kimoja baada ya vingine . Hapa ndipo unapaswa kujifunza kwa mataifa yaliyowekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu mfano Iran, North Korea walioishi na vikwazo kwa zaidi ya miaka 40+ ujifunze ni wapi wanashinda hivyo vikwazo na ni wapi hivyo vikwazo vinawaumiza vibaya Sana . Ili wewe usifanye makosa Kama ambavyo wanafanya wao kupelekea vikwazo kuwaumiza. Urusi anahitaji wasomi wake wakiuchumi kuumiza vichwa vyao kadiri wawezavyo ili mbio ndefu za kupambana na vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mingi waweze kuvishinda Kama ambavyo Sasa umoja wa ulaya Wana tafuta na kusaini mikataba mbalimbali ya kuuziana rasilimali [ gas, mafuta, makaa ya mawe ] na mataifa mengine ya mashariki ya Kati na Afrika ili kupunguza na Kama ikiwezekana ni kuondokana kabisa na kuitegemea Urusi kwa rasilimali hapa Urusi ni lazima atake asitake lazima azidishe ushirikiano na China, India, Brazil na anapaswa kuongeza washirika kwa mataifa mbalimbali ya Asia yaliyo bora kiuchumi n
ili kuweza kuuokoa uchumi wake na kuweza kushinda vikwazo vya kiuchumi kwa mbio ndefu pasipo kuwaathiri kwa kiwango kikubwa au kutowaathiri kabisa.

* Mwisho wa siku Kama tunakubaliana kuwa vikwazo vya kiuchumi vinawaumiza wao wenyewe ulaya walio viweka pia tunapaswa tuwe tayari kuyakubali matokeo hasi yatayo ikumba Urusi kutokana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa . Iwe ni matokeo hasi ya muda mfupi [ short run ] au matokeo hasi ya muda mrefu [ long run ] maana vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi ni vingi{ rundo } na vikali Sana.

-Ni hayo tu mkuu niliyonayo labda Kama na wewe utaweza kuongeza mengine.

kila mtu vinamuathiri lakin russia [emoji635] vinamuathir zaid ndo mana hajaweza kususa kupeleka gas Ulaya maana nae hana uwezo wa kufanya counter attack kwa kuwanyima gas.
maana hana njia nyingine ya kusurvive.
Angekua nayo angekua wakwanza kuitumia.
 
kila mtu vinamuathiri lakin russia [emoji635] vinamuathir zaid ndo mana hajaweza kususa kupeleka gas Ulaya maana nae hana uwezo wa kufanya counter attack kwa kuwanyima gas.
maana hana njia nyingine ya kusurvive.
Angekua nayo angekua wakwanza kuitumia.
Kingine ni kwamba hao north Korea na Iran wamehimiri vikwazo sawa lakini hawako kwenye vita ya Moja kwa Moja na taifa lolote kama ilivyo urusi, urusi kapigwa vikwazo,halafu wakati huo huo anatumia mabilion kila siku kufadhili vita vyake huko Ukraine,hapo lazima uchoke tu,
 
Hakuna first world country yeyote ambayo wananchi hawalalamiki, they are too much demanding. Mfano kichomuondoa Waziri Mkuu wa Italy ni nini hasa, kinachomuondoa Boris Johson pale UK ni kufanya party kipindi cha COVID-19 wakati kuna sanctions. Sababu ambazo ungekuwa Russia ukazisema unafariki bahati mbaya baada ya kuteleza na kudondoka kutoka dirisha la apartment yako huku mkeo akifariki bahati mbaya hapohapo baada ya kujikaba
hahahaaa huo ndo ukwel
 
Uchumi WA Rusia utayumba lakini hautaporomoka kama west walivyotarajia Kwa vikwazo walivyowekewa Rusia ulaya na Marekani walijua Kuwa Rusia hii vita hata kwenda nayo miezi ata mitatu haitafika ata Rudi nyuma ili kulinda uchumi wake Ila matarajio yamekuwa tofautii na Hali ikiendelea ivi kuna hatihati wakalamba matapishi Yao Kwa kuondoa vikwazo walivyoweka wao wenyewe hasa upande WA gesi, mafuta, mbolea,chakula, makaa ya mawe na vipuri hatari za kiuchumi mbeleni ni kubwa snaa Kwa ulaya kuliko Rusia utulivu WA Rusia kwenye kushughulikia ivi vikwazo limekuwa Jambo la faida sana kwao hawakurupuki wanafanya kama hawataki
Ulaya walikuwa wanaiona Rusia kama nchi ambayo walikuwa hawahiitaji kwenye uchumi wao Ila Kwa yanayotokea saivi kwenye chumi zao naisi ni ngumu kuitenganisha ulaya na Rusia
usiziamini serikali za kidikteta , kiduku alisema hakuna korona mpk ilipompata the same kwa Rais wa brazil
 
Malengo yake yakifikiwa wala hatajiweka kwenye hii vita sana akikamilisha eneo ya donesk kulimiliki atapunguza hii operations Kwa asilimia kubwa naona vita kubwa ikienda kupiganwa pale Odessa na inaweza kuchukua ata miezi miwili kama wakiimiliki basi itabaki kuzuia mashambulizi ya Ukrein wengi wanaichukulia Rusia kama pilipili hoho Ila bado ana uchumi imara pamoja na vikwazo vyote walivyopigwa
toka km 11 kuingia kyiev had mipango ya Odessa , Hongera Andunje Putin unajua kutufurahisha , mwaka tutakuwa tubapigana kuingia Crimea
 
Malengo yake yakifikiwa wala hatajiweka kwenye hii vita sana akikamilisha eneo ya donesk kulimiliki atapunguza hii operations Kwa asilimia kubwa naona vita kubwa ikienda kupiganwa pale Odessa na inaweza kuchukua ata miezi miwili kama wakiimiliki basi itabaki kuzuia mashambulizi ya Ukrein wengi wanaichukulia Rusia kama pilipili hoho Ila bado ana uchumi imara pamoja na vikwazo vyote walivyopigwa
Sio kweli bia tamu. Wazungu wa kimarekani uwezi gombana nao ukapona kiuchumi

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kupanda mchongoma Kushuka ndio Ngoma. Wachinjaji walienda Machinjioni kuchinja Ngombe walipo fika wakakuta Ngombe wameshika Visu na Kuwasubiri wachinjaji.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha YALE nchini Marekani wanasema uchumi wa Urusi unakabiliwa na uharibu mkubwa kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi, licha ya Moscow kupuuzia athari hizo.

Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa kazi yao inatilia mashaka madai ya Moscow kuwa uchumi wake bado uko imara na kuwa nchi za Magharibi zinaumia Zaidi kupitia kile kinatajiwa kuwa ni "vita vya kuzorota uchumi.”

Utafiti huo wasemaje?

Timu ya watalaamu wa Yale ilitumia data ya watumiaji bidhaa na takwimu kutoka washirika wa kimataifa wa kibiashara na usafirishaji bidhaa wa Urusi, kupima shughuli za kiuchumi miezi mitano baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini UKRAINE [emoji1255]

Waligundua kuwa msimamo wa Urusi kama muuzaji wa bidhaa ng'ambo umeyeyushwa kabisa, baada ya kulazimika kugeuka kutoka kwa masoko yake makuu barani Ulaya kuelekea Asia..

Utafiti huo unasema uingizaji wa bidhaa nchini Urusi umeporomoka tangu vita vilipoanza, na nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za kununua pembejeo, vipuri na teknolojia.

Timu hiyo iligundua kuwa uzalishaji wa ndani wa Urusi umekwama kabisa na haina uwezo wa kujaza nafasi za biashara zilizoanguka. Watayarishaji wa ripoti hiyo wanasema hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa na hasira ya watumiaji.

Nchi zaMagharibi zimeiwekea Urusi vikwazo. Huku kukiwa na karibu kampuni 1,000 za kimataifa zilizofunga milango yao nchini humo, Urusi imepoteza kampuni ambazo zinawakilisha karibu asilimia 40 ya patojumla la ndani kwa mujibu wa utafiti huo.

Ripoti hiyo imesema Putin anaingilia kati kwa kutumia njia isiyo endelevu ya kifedha ili kuficha mapungufu ya muundo wa kiuchumi.

Iliongeza kuwa bajeti ya serikali ya Urusi imetumbukia katika nakisi kwa mara ya kwanza na fedha za Kremlin zipo katika hali ngumu mno kuliko inavyoeleweka kawaida.

Wakati huo huo, watafiti hao wamesema masoko ya kifedha ya Urusi – wakiweka jicho kwa utabiri wa usoni – ndio yanayofanya vibaya Zaidi ulimwenguni, hali inayopunguza uwezo wa kuvutia uwekezaji mpya wa kuufufua uchumi.

"Tangu uvamizi huo, takwimu za kiuchumi za Kremil zimekuwa za kuchaguliwa, kwa kutoa maeneo ambayo hayaonekana kuwa mazuri kwao na kuchapisha tu yanayowafaa” unasema utafiti huo.

Urusi imewekewa vikwazo vya mafuta
Takwimu mpya za uzalishaji wa viwanda wa Urusi kwa mwezi Juni zinaonyesha kuwa iliathirika pakubwa katika sekta nyingi ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa magari, uzalishaji ulipungua kwa asilimia 89 wakati kwa nyaya za mawasiliano ulishuka kwa karibu asilimia 80. Nini kinachofuata kwa uchumi wa Urusi?

Waandishi wa utafiti wa Yale walisema Urusi haina mbinu ya kujiondoa katika janga hilo la kiuchumi kama washirika wa Magharibi wataendelea kuungana kuhusu vikwazo.

Utafiti tofauti wa Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama uliochapishwa Juni pia unaashiria kuwa uchumi wa Urusi upo kwenye misukosuko mingi, licha ya kustahimili siki za mwanzo za kutangazwa vikwazo.
"Athari za vikwazo ndio zimeanza tu kushuhudiwa: matatizo ya uzalishaji na usambazaji yanaongezeka na mahitaji yanapungua kwa kasi.” "katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.” Ilisema ripoti hiyo.

Source DW. Aljazeera

=========

NB: Russia kuomba msaaada wa kijeshi IRAN ni ishara tosha.

by the way tutauamini huu utafiti hadi tutakapo pata utafiti mbadala toka russia [emoji635]
Huawei mobile company ilipambana na USA kuhusu 5g. Sasa ivi hii kampuni imeanza kupungua kusikika apa duniani. Nadhani inapoelekea ishafika kibra

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Russia imefika ngapi?

Data za Nchi za magharibi si kila siku unazisoma mtandaoni, kuhusu uchumi wa Russia unapata taafifa zake kutoka ktk sources mbalimbali kama hao wa Ulaya na Magharibi?
Kama hamupati mlijuaje kwamba GDP ya RUSSIA sawa ba GDP ya jimbo moja huko yuesi ei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe, kwa pini alopigwa Russia sio rahisi uchumi wake kubaki imara kama ambavyo wanavyotudanganya.

Kampuni za Ulaya zilikuwa na ajira laki mbili kwa Warusi. Kampuni zaidi elfu moja zimeondolewa, bado nchi imepunguza mapato yake kupitia chanzo kikuu cha mapato ambayo ni Gas na Mafuta, na bado mtu anakwambia jamaa hawajatetereka.

Fikiria tu Tz hapa tuambiwe Utalii upigwe pini pamoja na sekta ya madini au Bandari, unafikiri tuna nini tena hapo?

Narudia tena, tunasema Ulaya inataabika kwa mfumuko wa bei kutokana na wao kuachilia huru vyombo vya habari, laiti Russia wakifungua vyombo vha habari viwe huru hapatashikika.
Aliokwambia kama GAS na WESE la RUSSIA mapato yamepungua nani !!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanao kimbia Russia sio wajinga wanakimbia na Mengi. vikwazo alivo navyo ni Nyokwe
 
Back
Top Bottom