Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,091
- 3,695
- Thread starter
- #61
Wacha na mimi nitie neno hapo mkuu, Vikwazo vya kiuchumi vina mbio mbili.
i, Mbio fupi[ short run ] na
ii, Mbio ndefu[ long run ]
- Kwenye mbio fupi{ short run }, mwanzoni kabisa mwa operation ya kivita ya Urusi nchi Ukraine baada ya Vikwazo kuanza Urusi ilitaka kushindwa Ila baada ya kukaa kwa wachumi wa ndani ya Urusi na kuweka mipango bomba wakaweza kushinda mpaka Sasa mfano kutoka kushuka kwa rubble na kupanda kwake haraka Sana mwezi wa tatu na hii kutokana na rubble Kutumika Sana kwa manunuzi baada ya Bank kuu ya Urusi kuamrisha malipo yote ya ununuzi wa rasilimali kutoka Urusi ni lazima rubble itumike Kama fedha kuu ya manunuzi na hapa umoja wa ulaya uliweza kushindwa na Urusi. Mpaka Sasa tunaona Urusi bado anasimama lakini si kwamba anasimama kwa nguvu Kama awali kabla ya Operation yake ya kijeshi kuanza huko Ukraine la hasha . Ana simama sawa lakini si kwa ubora Kama wa awali.
- Kwenye mbio ndefu{ long run } hapa inahitajika akili nyingi zaidi za wachumi wa Urusi kuliko hata mbio fupi hapa ni mbio za kuweza kuishi na vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu na huku ukivishinda kimoja baada ya vingine . Hapa ndipo unapaswa kujifunza kwa mataifa yaliyowekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu mfano Iran, North Korea walioishi na vikwazo kwa zaidi ya miaka 40+ ujifunze ni wapi wanashinda hivyo vikwazo na ni wapi hivyo vikwazo vinawaumiza vibaya Sana . Ili wewe usifanye makosa Kama ambavyo wanafanya wao kupelekea vikwazo kuwaumiza. Urusi anahitaji wasomi wake wakiuchumi kuumiza vichwa vyao kadiri wawezavyo ili mbio ndefu za kupambana na vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mingi waweze kuvishinda Kama ambavyo Sasa umoja wa ulaya Wana tafuta na kusaini mikataba mbalimbali ya kuuziana rasilimali [ gas, mafuta, makaa ya mawe ] na mataifa mengine ya mashariki ya Kati na Afrika ili kupunguza na Kama ikiwezekana ni kuondokana kabisa na kuitegemea Urusi kwa rasilimali hapa Urusi ni lazima atake asitake lazima azidishe ushirikiano na China, India, Brazil na anapaswa kuongeza washirika kwa mataifa mbalimbali ya Asia yaliyo bora kiuchumi n
ili kuweza kuuokoa uchumi wake na kuweza kushinda vikwazo vya kiuchumi kwa mbio ndefu pasipo kuwaathiri kwa kiwango kikubwa au kutowaathiri kabisa.
* Mwisho wa siku Kama tunakubaliana kuwa vikwazo vya kiuchumi vinawaumiza wao wenyewe ulaya walio viweka pia tunapaswa tuwe tayari kuyakubali matokeo hasi yatayo ikumba Urusi kutokana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa . Iwe ni matokeo hasi ya muda mfupi [ short run ] au matokeo hasi ya muda mrefu [ long run ] maana vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi ni vingi{ rundo } na vikali Sana.
-Ni hayo tu mkuu niliyonayo labda Kama na wewe utaweza kuongeza mengine.
kila mtu vinamuathiri lakin russia [emoji635] vinamuathir zaid ndo mana hajaweza kususa kupeleka gas Ulaya maana nae hana uwezo wa kufanya counter attack kwa kuwanyima gas.
maana hana njia nyingine ya kusurvive.
Angekua nayo angekua wakwanza kuitumia.