Yamungu Athumani
JF-Expert Member
- Apr 23, 2016
- 1,384
- 3,254
Usilazimishe Wote Tuikubari hiyo GSM yakoNiimejiridhisha pasi na shaka kuwa, wengi waliokuwa wanapinga udhamini wa (GSM) kwenye ligi na wote wanaosherehekea kujitoa kwake, wamegawanyika katika makundi makubwa mawili.
1...Hawajui katiba ya (TFF) hasa kuhusu suala la mkataba wenyewe unaotajwa kuwa ni wamagumashi.
2...Wanajua katiba ya (TFF), ila wanaendeshwa na hisia za ushabiki maandazi wa Usimba na Uyanga.
Kwanza kabisa hakuna sehemu yoyote ambayo (GSM) anamakosa kuhusu suala la udhamini mwenza kwa sababu yeye kama Muwekezaji alifuatwa na (TFF) akiombwa kuidhamini ligi kuu Tanzania bara na sio kwamba yeye alilazimisha kuja kuidhamini ligi.
- Jambo hilo lilithibitishwa na Rais wa (TFF) Wallace Karia ambaye alikiri kwamba wao kama (TFF) ndio walimuomba (GSM) aidhamini ligi kuu.
Baada ya (GSM) kuhakikishiwa na (TFF) + Bodi ya ligi kwamba logo yao itavaliwa na vilabu vyote (16) vya ligi kuu upande wa kushoto wa mkono wa jezi, na mabango yao yatawekwa kwenye viwanja vyote, (GSM) akakubali kuidhamini ligi....
... GSM kama kampuni wakakaa na (TFF) na bodi ya ligi wakafikia makubaliano ya kimkataba kuwa (GSM) watatoa Tsh 2.1 Billion kwa misimu (2) kwa awamu tofauti kulingana na makubaliano ya mkataba.
Kwa nini vilabu havikushirikishwa au vilishirikishwa ? Hilo sio jukumu la (GSM). Kwa mujibu wa katiba ya (TFF) wenye jukumu la kuingia Mikataba yote inayohusu Udhamini wa ligi, haki za matangazo ya Tv na radio nk ni (TFF)...
... (TFF) Wao ndio wanapaswa kusimamia vilabu ikiwemo kuwashirikisha na kuwajuza nini makubaliano ya Mikataba waliyoingia, japo katiba haiwalazimishi kufanya hivyo pia.
- Katiba ya (TFF) ndiyo iliyotoa LOOPHOLE ya baadhi ya vilabu kupinga Udhamini na sio (GSM)... Kwa kuwa (GSM) ni muungwana yeye ameamua kujitoa kwa sababu (TFF) imeshindwa kutekeleza makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana.....
.... GSM angeamua hata kuishitaki (TFF) kwa kumchafua au kwa kutotekeleza mkataba ambao uko kisheria. Lakini yeye akachagua kujiweka kando tu.
- GSM hapa anatumika kama kichaka cha kujifichia, lakini ukweli wa mambo ni kuwa Uyanga wake ndio unamponza kwa sababu kuna Mikataba mingi tu inayoingiwa hapo (TFF) bila kuvishirikisha vilabu kwa kutumia katiba hiyohiyo iliyopo lakini hakuna klabu hata moja ambayo ilishawahi kuhoji au kulalamika kuwa haikushirikishwa.
- Mimi naamini, kama huu huu mkataba wa Udhamini mwenza ungekuwa umeingiwa na kampuni nyingine tofauti na (GSM) kusingekuwa na hoja zoote hizo zilizoibuliwa kuupinga.
- TBC wameingia mkataba wa miaka (3) kwa Tsh 300 Milioni pekee, lakini hakuna klabu inayoyapinga mabango ya TBC kwenye viwanja kwa kusingizia kuwa pesa ni ndogo,, Lakini kwa GSM aliyetoa 2.1 Billion mabango yake uwanjani yalipigwa vita sana kwa madai pesa ni ndogo !!!!
Kikubwa Wamesepa na Wasepe
SIMBA HOYEEEE