Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

Niimejiridhisha pasi na shaka kuwa, wengi waliokuwa wanapinga udhamini wa (GSM) kwenye ligi na wote wanaosherehekea kujitoa kwake, wamegawanyika katika makundi makubwa mawili.

1...Hawajui katiba ya (TFF) hasa kuhusu suala la mkataba wenyewe unaotajwa kuwa ni wamagumashi.

2...Wanajua katiba ya (TFF), ila wanaendeshwa na hisia za ushabiki maandazi wa Usimba na Uyanga.

Kwanza kabisa hakuna sehemu yoyote ambayo (GSM) anamakosa kuhusu suala la udhamini mwenza kwa sababu yeye kama Muwekezaji alifuatwa na (TFF) akiombwa kuidhamini ligi kuu Tanzania bara na sio kwamba yeye alilazimisha kuja kuidhamini ligi.

- Jambo hilo lilithibitishwa na Rais wa (TFF) Wallace Karia ambaye alikiri kwamba wao kama (TFF) ndio walimuomba (GSM) aidhamini ligi kuu.

Baada ya (GSM) kuhakikishiwa na (TFF) + Bodi ya ligi kwamba logo yao itavaliwa na vilabu vyote (16) vya ligi kuu upande wa kushoto wa mkono wa jezi, na mabango yao yatawekwa kwenye viwanja vyote, (GSM) akakubali kuidhamini ligi....

... GSM kama kampuni wakakaa na (TFF) na bodi ya ligi wakafikia makubaliano ya kimkataba kuwa (GSM) watatoa Tsh 2.1 Billion kwa misimu (2) kwa awamu tofauti kulingana na makubaliano ya mkataba.

Kwa nini vilabu havikushirikishwa au vilishirikishwa ? Hilo sio jukumu la (GSM). Kwa mujibu wa katiba ya (TFF) wenye jukumu la kuingia Mikataba yote inayohusu Udhamini wa ligi, haki za matangazo ya Tv na radio nk ni (TFF)...

... (TFF) Wao ndio wanapaswa kusimamia vilabu ikiwemo kuwashirikisha na kuwajuza nini makubaliano ya Mikataba waliyoingia, japo katiba haiwalazimishi kufanya hivyo pia.

- Katiba ya (TFF) ndiyo iliyotoa LOOPHOLE ya baadhi ya vilabu kupinga Udhamini na sio (GSM)... Kwa kuwa (GSM) ni muungwana yeye ameamua kujitoa kwa sababu (TFF) imeshindwa kutekeleza makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana.....

.... GSM angeamua hata kuishitaki (TFF) kwa kumchafua au kwa kutotekeleza mkataba ambao uko kisheria. Lakini yeye akachagua kujiweka kando tu.

- GSM hapa anatumika kama kichaka cha kujifichia, lakini ukweli wa mambo ni kuwa Uyanga wake ndio unamponza kwa sababu kuna Mikataba mingi tu inayoingiwa hapo (TFF) bila kuvishirikisha vilabu kwa kutumia katiba hiyohiyo iliyopo lakini hakuna klabu hata moja ambayo ilishawahi kuhoji au kulalamika kuwa haikushirikishwa.

- Mimi naamini, kama huu huu mkataba wa Udhamini mwenza ungekuwa umeingiwa na kampuni nyingine tofauti na (GSM) kusingekuwa na hoja zoote hizo zilizoibuliwa kuupinga.

- TBC wameingia mkataba wa miaka (3) kwa Tsh 300 Milioni pekee, lakini hakuna klabu inayoyapinga mabango ya TBC kwenye viwanja kwa kusingizia kuwa pesa ni ndogo,, Lakini kwa GSM aliyetoa 2.1 Billion mabango yake uwanjani yalipigwa vita sana kwa madai pesa ni ndogo !!!!
Usilazimishe Wote Tuikubari hiyo GSM yako
Kikubwa Wamesepa na Wasepe
SIMBA HOYEEEE
 
Naskia lengo halisi lilikuwa kuitumia Simba SC, kutangaza bidhaa zao kimataifa.
Kwenye mashindano ya Shirikisho.

Kama Simba walikataa kudhaminiwa si wangezidhamini hizo timu nyingine ikiwemo timu yao ya Yanga.

Mkuu kuna vitu ukisikia uwe watulia na kutafakari...

GSM alikuwa anadhamini ligi ya NBC, na jezi anazotumia Simba kwenye ligi ya Bongo sio zile anazotumia kwenye mechi za CAF...

Sasa Simba angemtangaza vipi GSM kimataifa?
 
Mzima,kila siku vinailalamikia GSM hata kwa penati za mchongo wanazopewa wakikosa lawama kwa GSM
GSM katoa huo mzigo tff ili uje kuongeza nguvu Yanga,makolo match 13 penalty 8 goli za offside 7 halafu kila siku wanaleta propaganda za hata kolo akisikia mkewe kaliwa anailalamikia GSM
 
Acheni unafiki ipo siku zitatembea bakora hapo tifua tifua ndiyo akili itawakaa sawa
Tangu mkataba usainiwe Kati ya GSM na TFF na kushirikisha vilabu 15 ,vilabu havijapata mgawo ndani ya miezi yote mitatu .

Tulisema mkataba wa GSM ni wa kihuni na hawana huo ubavu kudhamini ligi , vilabu 15 vilijifanya vyote vimekubali na njaa zao na kukebehi Simba kumbe wanafanya matangazo ya GSM bure.

GSM ni genge la kihuni wamejaa chupli chupli tu.


View attachment 2111652
 
View attachment 2111982
Hayo ndio makubaliano ya GSM na TFF na wameshindwa Kuyatimiza, hata kama ni wewe mdhamini hauwezi hauwezi kutekeleza udhamini wako kama makubaliano ya kimkataba hayajatimizwa
Tuwe wa kweli...kama Mo angechukua nafasi ya GSM akaidhamini Ligi Kuu.. Unadhani Yanga wasingesumbua?!..Jibu ni hapana..Mpira wa Bongo bila kuzisikiliza hizi timu mbili TFF haina nguvu..
Hata kama walichofanya Simba kisheria na Kikanuni wamekosea,kilitegemewa tu, na Yanga wangefanya hivyo hivyo mdhamini angekua Mo..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Kwanza vigodoro vyake vina material mabovu afu ukilalia vinakuotesha ndoto mbaya ukiamka umechoka

Watu wengi wanaolalamika kwamba wachawi wamewalimisha usiku ukichunguza wengi hao wanatumia magodoro ya GSM
[emoji23]
 
Sasa vilabu vingepata vipi mgao wakati kulikuwa na mgogoro wa kimkataba?

Simba hakuwa tayari, hadi hapo GSM asingeweza kuendelea na mkataba na TFF...
Kwa hiyo shida yake ni Simba?
 
Basi asingeendelea kuweka mabango uwanjan na kuwapa taarifa vilabu kuwa wasivae nembo had swala litakapokuwa sawa.

Huo Ni uhuni timu zimekutangaza miez mitatu alafu unajitoa bila kuwalipa chochote.

Hii ngoma Bado mbichi GSM lazima wacheue pesa ya miez mitatu
Magodoro hayauziki atalipa na nini
 
Masharti ya mkataba yalifatwa. Ww timu yako ilikataa kuitangaza GSM[emoji2] haukuw mkataba unaoiacha Simba na kuhusisha timu zingine pekee.
Kwa hiyo mlikuwa mnaitaka Simba hahahaaaaaaa godoro limelowa maji..
 
Back
Top Bottom