Vimbwanga na Visa vya mahusiano ya JF

Vimbwanga na Visa vya mahusiano ya JF

Kuna jamaa anajiita smart sijui wamepotelea wapi na yule demu wake, jamaa ilikuwa kila akicoment lazima amutagi demu wake
 
kuna mtoto hapa namuelewaga sema ndiyo hivyo tena nahofia atanipa za uso
Sasa mkuu mtandaoni huku unaogopa za uso je mtaani kwako si unawakimbia kabisa, hebu jikaze mpe ya moyoni mwanaume inatakiwa uwe na ujasili.
 
Nilikutana na mtu humu tukachart kweli for al most 5 months picha nilizokuwa nimetumiwa sizo zenyewe. For more months to come finally video chart kumbe sio mwenye zile picha kazi na kila kitu alicho kisema sio so chakufanya nikumdelete tu.

Mwingine kasema i am single and i was finish in every thing. For 2 months tulivyokuwa tunachart his married. Another round is kukutana na mtu live but later anakuwa humuelewi.

NILIWAZA NIKAONA HIVI MAPENZI YA MITANDAONI NI KUWASTE TIME SERIOUSLY. WAPO WALIOWIN WAPO WALIOUMIA MIMI SIJAUMIA ILA NIMEJUA KUWA HUMU LAZIMA UWE MAKINI.
Ulivyoandika sasa
 
Kuanzisha mahusiano na mtu jf huku ukitarajia jambo flani kwa mtu uliyeanzisha nae mahusiano hayo inataka umakini na utulivu mkubwa.

Humu kunawatu wa aina zote ila wengi wao wanajielewa na wanauwezo wa kuwaelewa wengine.

Ukianza ukaribu na mtu, huishi salam kuonesha unajali ili kuweka ukaribu, usitegemee kitonga. Ndio maana wengi wanaokuja na malengo hayo huja na new ID

Uwelewa wako unapimwa na maneno yako" zitapitiwa threads na comments zako zote ulizowahi kutupia humu ili kujua utimamu wako kichwani.

Kwenye kutafuta rafiki,mwenza au kuamuwa nani wa kuwa nae kila mmoja huwa na vigezo vyake, ila hapa jf wengi huangalia mental attitude yako, nahii inatazamwa kwenye maneno yako on public sio pm kisha personality yako.

Kuna wakati mahusiano huwa yanakuja yenyewe pindi unapoamuwa kukaa kwenye position yako.
 
Back
Top Bottom