Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa mara nyengine Hamas itaachia mateka 4 wa Israel iliowachagua ambapo tayari majina yao yameshawekwa hadharani.
Jumamosi iliyopita ilikuwa ni burudani kubwa kwa ulimwengu na kwa watu wa Gaza waliposhuhudia kundi la Hamas likiwa limevalia kombati za kijeshi na kubeba bunduki walipojitokeza kwenye vichochoro vya kifusi huku wakikabidhiana mateka na Israel.
Burudani hiyo ilitokana na dhana iliyojaa kwa walimwengu wote kwamba kundi hilo lilikuwa limepotea kabisa baada ya vita vya zaidi ya mwaka mmoja.
Soma Pia: Hamas waeleza sababu za kuchelewa kuachiwa kwa kundi la pili la mateka
Yawezekana mateka hao walikuwa wameshikiliwa maeneo ya kusini au kati ya Gaza. Hata hivyo Hamas walichagua kufanya makabidhiano kwenye mji mkuu wa jimbo hilo unaoitwa Gaza city ambao ulikuwa umemiminiwa moto mkali wa makombora ya mfululizo kutoka angani.
Wafuatiliaji wa vita hivi kote duniani siku ya kesho watapenda kuona Hamas wamechagua eneo gani la makabidhiano hayo na zawadi watakazotoa kwa mateka hao wanne.