Triple G
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 3,018
- 4,369
Kwamba Baraka zilihama kutoka kwa Mdogo mtu kuja kwa dada mtu..!Yakobo wa kwenye Biblia😀😀
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwamba Baraka zilihama kutoka kwa Mdogo mtu kuja kwa dada mtu..!Yakobo wa kwenye Biblia😀😀
NI JASIRI Sana sana,,,,,wala hujakoseaAma Kweli wewe Yakobo katika Nyumba ya Labaniii
Ila dada mtu nae jasiriiii sana
wamama wa kirombo wapambanaji kwakweli......... so Siri Noah ScribeNI JASIRI Sana sana,,,,,wala hujakosea
Ukiangalia kwa jicho la tatu...kila kitu kwenye hii dunia Mungu ndiye anayepanga........
Ndiyo maana nawashauri vijana kwenye kuoa wasiumize vichwa.....MKE NI MUNGU NDIYE ANAYETOA......
NI JASIRI Kwenye kila kitu........na kimsingi tumevuka nae kwenye hali ngumu sana katika hii dunia......kuna wakati tulifulia sana sana,,,mpaka tukawa tunauza gongo nyumbani.......na POLISI akawa anapambana nao...
NItaendelea kuna kipengele chumba nilichopanga mama mwenye nyumba akaanza visa....sababu nae alikuwa na mabinti na kabla sijamleta huyu mrombo wao ndio walikuwa wanafaidi mkaa na mazaga ya safari.........Hapo ndipo nilishuhudia duniani kuna uchawi ....wachawi...na washirikina na walogaji tena wazi wazi......Mbona umeishia njiani bwana Yakobo 😹
Uliamua kumpenda hivo hivo? Ila wababa wa humu kwa mitungi 😜😜😜Nilikuwa kijana sasa ni mzee. Miaka hiyo nafanya kazi kwa kijana mwenzangu ambaye Mungu alimbariki na kumuinua sana kiuchumi kwa nyakati hizo. Ni kati ya Waafrika wa mwanzo kumiliki SCANIA 111 na 81.
Basi mimi akanikabidhi SCANIA 81 kwa roho safi (mtama kwa watoto). Nyakati hizo kazi ya lori inalipa kweli kweli – mixer "pofo", wizi wa dizeli, kubeba mizigo njiani, hakuna mizani, na makandokando mengi kama zama hizi za GPS, machawa, wapambe, na wakuu wa kazi.
Enzi hizo kujua Kiingereza cha kuombea maji cha zis and zat, tukawa na access za kuingia Gymkhana Club. Huko tukakutana na viongozi mbalimbali na tukajua mengi kupitia mvinyo. Kwa kifupi, huko ndipo tulipata kazi mbali mbali na mizigo ambayo tulilipwa fedha nyingi mpaka tajiri bosi wetu akawa anashangaa na kuzidi kutuamini. Mungu amlaze mahali pema peponi, AMEN (hakika wema hawadumu).
Sasa siku moja tukapata mzigo wa kupeleka Rombo. Ilikuwa ni vifaa vya ujenzi. Basi Mungu jalia tukasafiri salama mpaka Rombo. Daah, tulipokelewa kama wafalme. SCANIA mpya 81 imetinga Komangulwa. Tukakarimiwa sana – mbege swaafi, kisusio, na kama kawaida BLANKET CHAPA NTU.
BLANKET hili kumbe lilikuwa jipya na mimi kipindi hicho ndio natafuta mke. Nikaona mashallah huyu nitamtorosha. Kumbuka enzi hizo mtindo wa kuoa ni kutorosha na kutoa taarifa. Yaani unatafuta ka mbuzi fulani unakafunga pale nyumbani kwao. Pakikucha, wazee wakiona mbuzi, hawahangaiki kutafuta binti yao. Wanakuwa wameuelewa ujumbe.
Binti alikuwa amemaliza darasa la saba – alikuwa ni chuma kweli kweli. Sasa mpango wa kumtorosha ulihusisha baadhi ya ndugu akiwemo dada yake. Kumbe bwana dada yake ana lake moyoni. Akaona, "Yaani mdogo wangu anaolewa mimi niko hapa? Haiwezekani." Akaamua kupindua meza na kupeleka taarifa za uongo kwa mdogo wake.
Sasa mimi nikawa sehemu X napakia mzigo nikitegemea mdogo mtu ndiye anakuja. Hapo mabegi yalisha tangulizwa. Ebo, sina hili wala lile, naona mtu kajitanda khanga anajongea kwenye gari. Nikaenda kumfungulia mlango, akachoma ndani. Tena alikuwa amesindikizwa na kina Bwashee.
Nikaona isiwe taabu. Kina Bwashee nikawapoza, manake Bar haikuwa mbali na mimi nilikuwa nishachangamka kimtindo. Nikapasha gari, safari ikaanza. Haoo, mpaka Mombo. Nikatafuta guest. Binti kaingia chumbani, namuagizia kila kitu. Mimi nipo Bar naendeleza mvinyo.
Nikaingia chumbani, nikajiandaa kwenda bafu. Miaka hiyo bafu nje. Nae bado kajitanda khanga, namsindikiza bafu. Halafu unamsubiria kwa nje. Bado kajitanda khanga. Karudi ndani, bado kajitanda khanga. Na mipombe yangu nikaamua kula mzigo. Duuh, nikaona hii nyumba mbona kama tofauti? Sikujali sana.
Palipokucha, NDIPO NIKAGUNDUA KUMBE NI DADA MTU!
Kwa kifupi, nikamkumbuka Yakobo wa kwenye Biblia. Nikajua hili jambo si bure, kuna Mungu ndani yake. Nikaamua kuendelea naye na safari huku nikiendelea kumsoma. Kwa kifupi, huyu ni mama wa Kirombo. Ni jembe kweli kweli.
Nikamwacha kwenye chumba nilichokuwa nimepanga wakati huo. Kila nikienda safari, nikirudi – mkaa labda gunia 2. Moja anasema tunauza, jingine ndio tunatumia. Kila nikibahatisha vijisenti vya safari nikimuachia, nakuta amebajetia vyema. Mara nyingine nafulia, yeye ndio anaokoa. Trip za njia ya kati naleta mafuta, kuku Singida, mchele wa Shinyanga.
Kwa vitu hivi vidogo vidogo, tulianzisha duka genge.
Kabisa..... bila yeye leo nisingalikuwa hapa.....nimeona mifano mingi kwa wenzangu....hasa wenye wanawake wa kwenda ngomani na kupaka kucha rangi...wamama wa kirombo wapambanaji kwakweli......... so Siri Noah Scribe
Mama zangu naelewa sana wana madhaifu mengi lkn kwenye ku hustle.... wako vyedii....Kabisa..... bila yeye leo nisingalikuwa hapa.....nimeona mifano mingi kwa wenzangu....hasa wenye wanawake wa kwenda ngomani na kupaka kucha rangi...
😀 😀 😀 😀 😀 KWa life ya sasa mitungi inaongeza siku mkuuUliamua kumpenda hivo hivo? Ila wababa wa humu kwa mitungi 😜😜😜
Pombe au waweza sema mipombeLugha zenu ngumu..'mitungi' ndio nini?
Sometimes inawaponza 😅😅😅😀 😀 😀 😀 😀 KWa life ya sasa mitungi inaongeza siku mkuu
Kama mimi apa sahizi naumwa juzi nimepata mrembo nikiwa mitungi sahzi najitibu kisonono,,,, ila hatuachi kwakweli tutakua tunapumzika tu.Sometimes inawaponza 😅😅😅
Mkuu umenitia moyo sana kwa kauli yako hiiNI JASIRI Sana sana,,,,,wala hujakosea
Ukiangalia kwa jicho la tatu...kila kitu kwenye hii dunia Mungu ndiye anayepanga........
Ndiyo maana nawashauri vijana kwenye kuoa wasiumize vichwa.....MKE NI MUNGU NDIYE ANAYETOA......
NI JASIRI Kwenye kila kitu........na kimsingi tumevuka nae kwenye hali ngumu sana katika hii dunia......kuna wakati tulifulia sana sana,,,mpaka tukawa tunauza gongo nyumbani.......na POLISI akawa anapambana nao...
aLifanya ujinga mkubwa sana,ingekuwa ni vijana wa sasa,wangemshusha hata kama keshamlaDada alimzibia dogo