Vimto kutoka Saudia ni kinywaji bora kama utaweza jaribu kunywa hutajuta

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1657284251347.png
Asili ya kinywaji hiki kilitengenezs mwa kwanza Manchester Uingereza miaka ya 1800+. Ni mchanganyiko wa berries na zabibu zilizosagwa pamoja na viasilia vingine.

Kinywaji hiki kilitumiwa sana na wanajeshi wakati wa WWI, walifungiwa mabox ya Vimto na kuoekekewa huko mstari wa mbele.

Miaka ya 1900+ waarabu walipata leseni ya kutengeneza Vimto na waliendelea kuitengeneza kwa ubora ule ule. Leo hii Vimto ya Saudia imebaki kuwa bora kuliko ile inayotengenezwa Uingereza. Arabuni kinywaji hiki ni maarufu hasa wakati wa Ramadhani baada ya mfungo wa siku nzima.

Kwa ubora wake changanya 100mls za Vimto kwenye jug la maji lenye ujuzi wa 500mls. Maji ya baridi yanafaa zaidi.

Si kuwa ninawafanyia promotion lakini ningependa kizuri tukinywe wote. Mbele ya Vimto ya Saudia huwa beer 🍺 siipi nafasi.
 
View attachment 2284531

Kinapatikana wapi?
 
Miaka ya 80 nilipokuwa huko ndio kilikuwa kinywaji changu bora kabisa na pia inakuja kwenye kopo pia ya 330ml ni tamu haswa Halafu iwe baridiiiii

Yaani na joto lile la 50 something degrees daaa umenikumbusha mbali sana ingawa naona kama juzi tu
 
Dubai maduka yote ya vyakula yaani supermarket.
Unakumbuka zamani kuna mhindi mmoja nadhani sasa ni marehemu, aliitwa Viran. Nadhani alikuwa mfadhili wa Yanga. Kiwanda chake kilikuwa kinatengeza na zilikuwa zinapatikana kwenye vichupa vidogo vidogo hasa maeneo ya Kariakoo. Sidhani kama zilikuwa zinafika mikoani.
 
Zilikuwa zinatengenezwa zamani hapa Tanzania na kiwanda cha mhindi mmoja akiitwa Viran. Kusema kweli kwangu ni kinywaji kizuri sana. Ukiinywa ya baridi wakati wa joto la Dar unapata burudani ya aina yake.
Hata Tanga wale Wahindi wa Khanbai Pharmacy walikua wanatengeneza concentrated syrup walitumia strawberries kutoka Lushoto. Sikuhizi hakuna vitu hivi tena.
 
Unakumbuka zamani kuna mhindi mmoja nadhani sasa ni marehemu, aliitwa Viran. Nadhani alikuwa mfadhili wa Yanga. Kiwanda chake kilikuwa kinatengeza na zilikuwa zinapatikana kwenye vichupa vidogo vidogo hasa maeneo ya Kariakoo. Sidhani kama zilikuwa zinafika mikoani.
Mama alininunulia sana hizi pamoja na skonzi ili njaa isiniadhibu shuleni.
Zilitufikia hata sisi wa mikoani.
 
Back
Top Bottom