Vineno vidogo vya Kiingereza vinavyosumbua baadhi ya wazungumzaji

Vineno vidogo vya Kiingereza vinavyosumbua baadhi ya wazungumzaji

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Kila lugha ina maneno fulani yanayosumbua wanaojifunza hiyo lugha. Nimegundua katika Kiingereza yapo haya maneno yanayotumiwa vibaya na baadhi ya watu kama ifuatavyo:

their, there, they are: Maneno haya mawili yanawachanganya sana baadhi ya watu.Nimeshakutana na matumizi yafuatayo ya maneno hayo kama:

1.The guests have come. Show them there rooms
2.Where are the cats? I see, they are their.
3. conflict: Baadhi huandika comflict wanapoitumia kwenye sentensi. Ugonjwa wa hili neno lenye herufi n pia upo kwenye neno convert ambayo huandikwa comvert. Hata hapa JF, kuna mdau kwenye jukwaa fulani ametangazia ufundi wake wa kubadili frdge kuwa incubator, ameandika: I comvert fridge into incubator

Chanzo cha tatizo:
Nionavyo,matatizo ya matumizi ya haya maneno yanatokana na matamshi yake.

Suluhisho:

1. Tutumie muda kuyapambanua hayo maneno kwa kuyakariri vizuri
2. Kila tunapoyatumia kwenye maandishi tuhariri maandishi hayo kuhakikisha tumeyatumia vizuri.

Nina uhakika yapo mengine kadhaa ambayo nimeyasahau. Mdau mmoja kwenye jukwaa hili kazungumzia loose na lose.
 
Their na there sio siri zinansumbua sana huwa nakua makini sana.
 
Sikiliza wasanii wa bongo fleva na bongo movies wakifanyiwa interview jinsi wanavyo changanya 'support na supporter'
Wasanii wa bongofleva ndo kabisaaa.Wanasumbuliwa sana na ufahamu wao finyu wa lugha ya kiingereza.Wao ni wataalamu wakubwa wa 'yaaa!, of coz, at least, .....'
 
kwenye vijiwe vya football, liko neno ambalo hata watu linawasumbua. Defence and defend.
Mfano: Timu ya Costa Rica inaji 'defence' zaidi.
Hilo tatizo la kuchanganya noun na adjective lipo sana patience96. Utasikia:Ipo different kubwa kati ya mkoa wa Lindi na Mtwara. nk.
 
Last edited by a moderator:
Kuna haya pia; stationery and stationary. salon and saloon, beep and deep pia it's and its
Asante DR. MWAKABANJE kwa kuniongezea orodha. Hiyo niliyobold ipo sana hapa Moshi kwenye vibao vinavyotangaza biashara/huduma za uchapaji na vifaa vya ofisi.
 
Last edited by a moderator:
professionalism...maana ya hili neno kwa kiswahili....
 
oke thenkyu vere macheeee.kwa sauti mama Anna Makinda.chezea kizungu wewe.
 
Back
Top Bottom