Vingunguti: Watu wawili wauawa kwa kupigwa na risasi

Vingunguti: Watu wawili wauawa kwa kupigwa na risasi

Hata iwe ni wezi hakuna justification ya kuua watu ambao hawana silaha. Jaribu kuingia YouTube usikiliza maelezo ya huyo kaka mtu ndiyo utajua ni mauaji ya kinyama. Wanasema polisi walikuwa wanafanya doria tangu mchana na walishawakamata na kuwaweka chini ya ulinzi. wakaanza kuwapiga risasi za miguuni na baadae mwilini tena mbele za watu. Mimi ndiyo maana huwa nasema watanzania tuko kama manyumbu. Mtu anaua na watu wanaona ni sawa tu.
 
Mahakama zimewekwa za nini? Utajua fulani ni mwizi bila kumfikisha mahakamani? Huoni utaratibu wa aina hii unatoa mwanya kwa polisi kuua mtu yeyote kwa kisingizio kuwa ni mwizi? Hivi kama mna ugomvi na mtu, na huyo mtu akampa polisi fedha nyingi ili akupige risasi kwa kisingizio cha kuwa wewe ni mwizi huoni unaweza kuuawa bila sababu?
Sijui kwanini watu hawaoni huu upande, mtu anachukuliwa mke na bodaboda, kijana wa bodaboda anauliwa unaambiwa alikuwa Panyaroad.
 
Back
Top Bottom