Mahakama zimewekwa za nini? Utajua fulani ni mwizi bila kumfikisha mahakamani? Huoni utaratibu wa aina hii unatoa mwanya kwa polisi kuua mtu yeyote kwa kisingizio kuwa ni mwizi? Hivi kama mna ugomvi na mtu, na huyo mtu akampa polisi fedha nyingi ili akupige risasi kwa kisingizio cha kuwa wewe ni mwizi huoni unaweza kuuawa bila sababu?