Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Tusio na watoto kwanza ngoja tuwe wasoma comments za wazazi
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Acha kiherehere narudia kukwambia.
Unasema mada ya kike it means watu wote wanaochangia hii mada ni wanawake huoni unatutukana? Alafu unataka ujibiwe vizuri ili iweje?
Acha kiherehere kama mada haikufai nenda jukwaa lingine mbona simple tu

Mada kama hii huwa zinaletwa na wanawake halafu wanaume ndio wanachangia.

Sasa kidume mzima unajipinda unaanzisha uzi kama huu....!!!!

Unatukosea sana wanaume wenzako.
 
du pole kama mimi tu watoto wachanga wanasumbua kweli
 
Mtoto wa dada yangu ana kama 8 month anapenda matangazo ya kwenye TV balaa.
Akisikia tangazo lolote hata kama ananyonya anaacha mpaka liishe
 
[emoji23] [emoji1]
 
Alizoea kutuona nyumbani tunatumia tochi kutafuta
kitu kama kimepotea na ni sehemu ya giza,
yeye kwa akili ya utoto akajua tochi ni dawa
ya kupata kitu kilichopotea.

Basi siku moja mchana akiwa nje anacheza
akapotelewa na mojawapo ya zana zake za
michezo,akarudi ndani na kuchukua tochi
alipoulizwa "wewe unapeleka wapi tochi"
akajibu "nimepotelewa na vitu vyangu nje naenda kuvitafuta"
Kweli utoto ni raha sana.
 
Hahah aisee. Safi sana
 
Dah...nimecheka sana sentesi ya mwisho
 
Yeye hataki kuula, anamlisha mdogo wake[emoji1]
 
Mtengenezeeni ubao wake.
 
Mmekutana[emoji1]
 
Mi wangu akisikia kile kitangazo cha "ammmka ammka" cha clouds kabla bonge haja ongea anaanza kucheza cheza yani hata kama kalala
 
Mtoto ni mtoto, umdhaniaye kuwa hatakuwa wa msaada kwa kuwa ni msichana, ndiye pengine atakayekuokoa. Cha muhimu ni kuwawezesha wote bila ubaguzi/upendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…