Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Ukongwe wako hautuhusu na hakuna aliyekuita uje kusoma huu uzi.
Ukisema ukongwe kila mtu ni mkongwe kwa mwenzake.
Usilete stress zako za maisha mkuu kama unaona uzi hauna maana tembelea jukwaa la ufugaji, siasa n.k

Sawa Dada.

Endelea kuleta stori za mtoto wako.
 
Kila mtu mtoto wake wa miaka 2 anajua kutumia computer.

Stori za dada zetu wakiwa salon hizi.

Yani naona kila mwenye mtoto utaskia nimtundu mala anaakili sana mala mjanja mjamja mala nini naona sifatu inamaana nyie wenye watoto wote hakuna mwenye mtoto zoba anae lialia nakulamba kamasi mdawote anae pigwa nakila mtoto humu hakuna du!!! Ebu ongeeni ukweli wenu msifate mkumbo
 
Aisee binti angu 1.8 ni maarufu mtaan kwetu(platnumz) halafu mkitoka nae matembezi hataki kushikwa mkono
 
Mengi sana, miaka 5, alivyokuwa na miaka minne nikawa nnnamfundisha kuandika sasa a anaandika kama q nikamwambia afute, akaniita jina langu, akaniambia ninamzingua

Hamna mtu atakaegusa kitu changu, kwake ni ugomvi mkubwa kushika kitu cha baba yake, hasa simu

Anapenda kuvaa vitu vyangu kama viatu n.k

Mkitoa out hamna kushikana mkono
 
Mmmmmh huko kumnenea mwanangu mabaya sintanena kamwe, labda ujisemee ww wangu jembeee
Hamna aliyemnenea mtoto wa mwenzie mabaya hapa
Ila uongo hausaidii kitu wewe mtu anakuambia mwanae Ana miaka 10 yupo form 3
Oooh! Mwanangu 2 yrs anajua sana kikorea na kompyuta na sijamfundisha
Achaneni kutuletea story zenu mnazodanganyana mkiwa saloon
 
Huu uzi unaanza kutamanisha [emoji28]
Francis Mawere kumbe bado??! Nikuazime wangu???!

Mi hata nashindwa kumuelezea Bebé wangu maana sofa zake zinajaa dunia!!

Juzi tu kametoka kunifurahisha na matokeo yake ya midterm maana kamepata
Kako smart, mtundu sana alafu ni mchokozi balaa. Sema uzuri wake sio muharibifu...alafu ishu ya uchokozi hats Mimi nachangia maana namwambiaga mtu akimuonea mara kwa mara nae aanze kumdunda, ila anapokuwa amechokozwa tu.

Sifa yake kubwa kabisa kubwa kabisa no kujali. Yani ma-hug na makisses mia moja elfu kwa siku. Hata ukiwa na stress zinaweza zikayeyuka tu jinsi anavyopetipeti.
 
8d65a875ed859e8de6b61117c2894bbd.jpg

Huyu anapenda mapicha kama msanii ukiacha sim utakuta kajipiga selfie zaidi ya 100 nacho mpendea ni mwerevu
Hamjafanana...umebambikiwa
 
Sawa Dada.

Endelea kuleta stori za mtoto wako.
Acha kiherehere mkuu, ukongwe wako haunihusu kwa sababu watu wote hatulingani mipando wala umri.
Unajifanya kunijua alafu unaniita dada we boya sana kama hujui jinsia ya mtu uliza usilete kiherehere hapa hujalazimishwa kusoma huu uzi.
 
Acha kiherehere mkuu, ukongwe wako haunihusu kwa sababu watu wote hatulingani mipando wala umri.
Unajifanya kunijua alafu unaniita dada we boya sana kama hujui jinsia ya mtu uliza usilete kiherehere hapa hujalazimishwa kusoma huu uzi.

Kwahiyo unataka kusema wewe ni wa kiume?

Unajua huu uzi umeka kike ndio maana nikajua hata wewe ni bint.

Samahani sana mkuu kwa kukukosea.

Ila siku nyingine usiwe unapaniki hapa JF tupo watu tofauti wenye mawazo tofauti.
 
Huyu dogo an 3Yrs

#1. Siku moja aliniambia "Baba nataka kuolewa"... Nikamuuliza unataka kuolewa na nani akanijibu " na wewe"..... Nikapigwa na butwaa.


#2. Siku nyingine akaniambia "Baba nina mimba".... Nikajifanya kama sijamsikia.


#3. Siku nyingine akaja na ua anaiambia "Baba ua la bibi harusi".

#4. Siku moja nilienda naye nyumbani akamuuliza baba yangu " Babu wazazi wako wapi?.... Baba akamjibu " wamefariki"... Dogo akasema "unaishi vipi bila ya wazazi".


Hayo ni machache

Hahahahahaaa looh I love your kid.

Hiyo namba 2. Imenichekesha mnoo aahahahahahaa ati nikajifanya sijasikia hahahahahahaaa natamani nimuone binti yako.

Mwanao ana ufikiri wa hali ya juu, usimpuuze. Jitahidi kuwa nae karibu na umjibu maswali yake. Usiache akaulize kwa wengine.
 
Back
Top Bottom