Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Binti mwaka 1.6 wimbo wa darasa maisha na muziki hata kama amelala lazima ataamka na kuucheza mwanzo mwisho
 
Wazazi wakongwe hayo mambo ni kawaida.

Wazazi wapya kila muda wanataka tusikilize stori zinazohusu watoto wao.
Ukongwe wako hautuhusu na hakuna aliyekuita uje kusoma huu uzi.
Ukisema ukongwe kila mtu ni mkongwe kwa mwenzake.
Usilete stress zako za maisha mkuu kama unaona uzi hauna maana tembelea jukwaa la ufugaji, siasa n.k
 
Sitochoka kuwatamani mapacha. Ee mungu nijalie mpacha nikibahatika kupata watoto

basi hapa ninapoishi mtoto wa mama mwenye nyumba kama wangu nampenda sana max.

Napenda anavyokuja kunigongea asubuhi kuniuliza kama nina uji, au akiwa na njaa uja na kuuliza kama nimepika wali,

nikienda safari au town basi siwezi sahau pipi au chohote maana nikifika anauliza nimemletea nini.

Nikiwa natoka kanapenda kunifata basi nikitoka nako wanasema mwanangu.

Nilipokuwa naishi awali huyu mama alikuwa na mapacha watatu jamani nilipenda kwenda kuwabeba nikifika na zawadi vinaanza kuniita amaa amaa amaaa.

Kitoto cha mdogo wangu dah huyu ndo funga kazi yaan kinanipenda utafikiri mm mdo mama yake aliwa mdogo kuna kipindi nililazimika kuishi nae basi nilipenda kumuimbia hili alale basi nitaimba nyimbo za kiruga mpaka asinzie.

Siku moja alinichekesha alikuta nimelala hapo kashakuwa 3yrs akasema "mama imbia wewe" nikasem imba" akaanza baby oh nana nana baby! Hapo ananipiga mgongoni nilicheka sana. Watoto watam
Tatizo unabana Sana. Huwezi pata HIV hiv
 
Mi wa kwangu balaa natamani akue kidogo labda nitapata zuri la kueleza, leo ni wiki ya tatu sijalala nakesha, dogo analala mchana wakati mimi nipo job, usiku halali na akilala mikononi ukimuweka kitandani tuu yani kabla hata hujakiacha kitanda kishaamka na kelele nyingi, kingine asee usikae karibu na mamaake ugomvi wake c mdogo atalia hapo hadi utashangaa, kingine tangu wiki iliyopita hajacheka sijui ndo kutabasamu hakuna. Ana miezi 4. Hataki kulazwa kama watoto wengine anapokuwa macho, yeye anataka kukaa na anakaa...huyo ni mdogo, kakayake yeye anapenda ngumi, anajua bunduki zote kwa majina, hili nimejaribu kumuonya mamayake asiwe akimuwekea movie za mapigano zaidi ya cartoon lakini sijui huyu kijana anajifunzia wapi maana hakawii kukwambia anataka awe mwanajeshi sababu hapendi majambazi, huyo Ana miaka mi 4, anajua kikorea, kajifunza wapi mi sijui...ila ana shida moja anapenda tambi tuu, vyakula vingine kula mpaka mpigizane kelele sana na husingizia anataka kukojoa akienda harudi..ana huruma sana na mamayake, mjanja mjanja sana ukikasiririka atajua jinsi ya kukufanya ucheke tuu, shida usimuache na mdogo wake peke yao, unaweza kuta mtoto analishwa ugali.
Nimecheka saaana. Mwanao km wangu ana miaka mitatu na miezi mitatu... Anapenda mikate ila anaitengeneza iwe muundo wa bunduki ndogo ndio ale. Kingine ukitaka umpw raja mnunulie gari na bunduki( kuna zile zinazorusha maji) atalitega gari na kuanza kulilipilia mabunduki yaaani..
Being a mother is a wonderful experience.
 
Mwanangu alipokuwa ba miaka 1-2.5 hivi yaani alikuwa akisikia baba yake anaonngea kwa nguvu alafu ananiangalia anaenda kumpiga.. Nikienda nae salon km msusi anavuta nywele nikikunja sura anaenda kumpiga... Alikuwa ananilinda sana. I love him kwa kweli.
 
akilala dizain analala kama mbuzi kagoma ..hahahaha bas burudani kwel kwel..
ilo poz ndo lazma aanze kutafutia usingiz...
 
Naombeni kujua kuna mtoto wa jirani yangu ana 3yrs lkn hawezi kuongea hiii itakuwa ni nn na afanyaje ili mtoto wake aweze kuongea?

Naombeni msaada wenu tafadhali

Mkuu unaweza kupitia hiyo link ukapata majibu, ukikwama niulize.

Ankyloglossia - Wikipedia

300px-Frenulum_linguae.jpg
 

Attachments

  • upload_2017-6-8_18-57-7.jpeg
    upload_2017-6-8_18-57-7.jpeg
    5.8 KB · Views: 46
aise watoto ni raha sana.uyu wakwangu mdogo mwenye mwaka 1na miezi 8 sitaki kabisa akue kwa vituko anavyonipa.yaani ningekua na uwezo wakuzuia ujuaji wake ningefanya ivyo kwa kweli.yeye katuni anaita kukuti na anakatuni yake moja anataka iyo iyo iwekwe siku nzima.ukibadilisha tu vi ugomvi.akishasema kukuti kuwe na umeme kusiwe yeye ilo hajui ata taarifa ya habari imekua shida kuangalia.ila sasa hivi nimemuweza,nimemtafutia mtumba wa laptop kupunguza kelele.

hahaha mkuu pole tafuta ata chogo la 21 inch mkuu ...litamfaa mfungieni ka corner kake...mum limit tu distance na mda
 
Mwanangu (5yrs) yeye bwana computer... Ameanza kuijua kila kona ya computer akiwa na miaka kama 2 hivi.. Saiz hashikiki kwa kuitumia iwe ni games zile za mission au kuset tu vitu mbalimbali.. Kuna vitu vingine nimemfundisha ila vingi amejifunza mwenyewe.. Kipindi cha nyuma ilikuwa kila wiki na weka Windows upya ikabidi nimtaftie tu computer yake saiz mzee kuna siku siku nikamkuta kashika bisibisi kashafungua laptop nati mbili nyingine zimemgomea kisa iligoma kuwaka.. Kuna siku nikasahau external hdd kutoka kazini kikakuta pc yake imejaa ka install kila game na software iliyopo ndani yake..
 
Yani naona kila mwenye mtoto utaskia nimtundu mala anaakili sana mala mjanja mjamja mala nini naona sifatu inamaana nyie wenye watoto wote hakuna mwenye mtoto zoba anae lialia nakulamba kamasi mdawote anae pigwa nakila mtoto humu hakuna du!!! Ebu ongeeni ukweli wenu msifate mkumbo
 
Haya mambo ya wazazi kutopata muda wa kukaa na watoto wao, kuna dogo aliharibu ndoa ya wazazi wake, bila baba wala mama kujua kwamba dogo miaka 4 ameshajua kusoma vizuri alichukua simu ya baba yake, sasa bahati mbaya sijui ilikuwaje wakashtuka anasoma meseji ya mchepuko kwa kwa sauti mpaka akaimaliza, ma mama alikuwa hana tabia ya kugusa simu ya mume wake.

Kilichoendelea hapo ni mtafaruku.
 
Wangu ni vijana wa Mwenye Enzi Mungu Mwenyewe, anawafundisha na kuwa Linda na kuwabariki Mwenyewe! Mimi wala baba yao hatuna cha kujisifia juu yao, sifa zote ziende kwa Muumbaji wa vitu vyote kwa kweli!
 
Usije ukaanza kumlazimisha asome awe daktari au mwanasheria hicho ni kipaji tayari anacho kitamtoa aongezewe tu elimu kiasi sio madegree ili mzazi ujisifie.

Hongera sana Mkuu
Asante mkuu.

Yes, sina mpango wa kuwalazimisha watoto wangu chochote.

Kwanza nawalea kisela. Tunaenda kishkaji mpaka.sometime huwa najishuku mwenyewe.

Am I wrong.
 
Back
Top Bottom