Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Yuko na mama yake huko anakopiga job (as no uhamisho) ana 2.6 yrs siku mbili mfululizo kagoma kila kitu anataka amwone baba...nikipiga simu analia tu na kusema njoo huku haraka, niletee mkoba na peni!!!!
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
Mtafute huyo mtoto ndugu yangu..

Hakuna raha kama kucheza na kuwa rafiki wa watoto wako..

Mnawakosea haki sana watoto nyinyi watelekezaji.
 
Ana miezi 5 yeye hata akiwa analia jifanye unaongea na simu ananyamaza kusikiliza maongezi ukiacha tuu anashusha kilio....anapenda sana kusikiliza maongezi ya simu hata kama anasinzia ataamka
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Aisee mie sitaki hata kukumbuka,mwanang alikuwa mtundu balaa at least sasa hivi nimepumua,wakati akiwa na miaka mitano akiwa shuleni (boarding) sijui alitoa wapi mfuko ule wa Salfeti akawachukua watoto wadogo watatu akawafungia kwenye mfuko halaf akawaambia atakayepiga kelele namchapa viboko,akatoka akaenda kucheka bahati nzuri mwalimu akapita pale akaona mfuko unacheza cheza akashangaa kuufungua akakuta watoto walishaanza kuchoka, huku na huku nani kafanya hivi wakamtaja,mwalimu wake ananipigia simu mwanao leo kafanya kosa hili yaani nliishiwa pozi, nkaenda shuleni kwao namuuliza akanambia ahaa niliwaweka watulie maana walikuwa wanasumbua,siku nyingine karudi likizo niko kazini , akaweka Cd tano kwenye radio inayobeba cd tatu, nilivyorudi kanipokea getini akanambia yaani Mom radio yako imegoma kabisaa kuimba leo ahaa itakuwa ulinunua radio ya kichina,nafungua pale kaweka cd kushinda uwezo na sijui alichokonoa nn radio ikafa kabisaaaa
[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
Tuliotelekeza mimba haituhusu hii
images-14.jpg

Na hali kama hii ndio baadae huwakuta hao watoto mnao watelekeza mimbani
 
Wakwangu anamiaka 4 juzi kaniuliza baba nani kamzaa shetani
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Mwanangu (5): Baba mbona unapunguza mwendo??
Mimi: Kuna askari mbele
Mwanangu: Sasa usipopunguza mwendo atakufanyaje?
Mimi: Atanikamata
Mwanangu: Atakukamata atakufanyaje?
Mimi: Atanifunga kamba anipeleke gerezani kunifunga.
Mwanangu: Police kazi yake kufunga kamba watu?
Mimi: Ndiyo, ila wale wakorofi tu.
Mwanangu: Hata watoto wadogo anawakamata na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo, lakini wale watoto wakorofi wasiopenda kufanya H/W
Mwanangu: Mimi si mkorofi na nafanya HW, si ndiyo baba
Mimi: eeeee
(Tunawakaribia Police wa usalama barabarani tunawapita)
Mwanangu: Police nimewaona watatu pia kuna Mwanamke, baba hata Police Mwanamke yupo
Mimi: Ndiyo
Mwanangu: Na yeye anaweza kukamata watu na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo:
(Ukimya dakika 2)

Mwanangu: Baba weka speed One hundred tumeshawapita ma police. (huku akiangalia mshale wa speed-meter)

-------------
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji14]
 
mie wangu ndiyo ameanza shule, basi nina kibarua cha kuimba nyimbo za shuleni kila akirudi. kupewa story za madam wake sijui anko.

na mbaya zaidi kupigiwa ngoma ili niimbe nyimbo ya Taifa. hapa uwa nachoka sana aiseee.

kingine kila mahali panachorwa sasa hivi, ukuta imebidi tuulinde kuliko kitu kingine.
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
aise watoto ni raha sana.uyu wakwangu mdogo mwenye mwaka 1na miezi 8 sitaki kabisa akue kwa vituko anavyonipa.yaani ningekua na uwezo wakuzuia ujuaji wake ningefanya ivyo kwa kweli.yeye katuni anaita kukuti na anakatuni yake moja anataka iyo iyo iwekwe siku nzima.ukibadilisha tu vi ugomvi.akishasema kukuti kuwe na umeme kusiwe yeye ilo hajui ata taarifa ya habari imekua shida kuangalia.ila sasa hivi nimemuweza,nimemtafutia mtumba wa laptop kupunguza kelele.
 
watoto ni faraja sana wangu ana 1.5 analipenda lile tangazo la cocacola hata akiwa mbali vp akisikia tu anakuja.. Anavoitamka cocacola ss... Ndo kichekesho
Wa kwangu ameanza kulipenda ilo tangazo akiwa na miezi mitano hata kama ungekua analia likianza anajipa break ya kulitizama likiisha anaanza upya na program yake ya kulia ila mpaka Leo ana 1.1year still analipenda
 
Back
Top Bottom