Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Sitochoka kuwatamani mapacha. Ee mungu nijalie mpacha nikibahatika kupata watoto

basi hapa ninapoishi mtoto wa mama mwenye nyumba kama wangu nampenda sana max.

Napenda anavyokuja kunigongea asubuhi kuniuliza kama nina uji, au akiwa na njaa uja na kuuliza kama nimepika wali,

nikienda safari au town basi siwezi sahau pipi au chohote maana nikifika anauliza nimemletea nini.

Nikiwa natoka kanapenda kunifata basi nikitoka nako wanasema mwanangu.

Nilipokuwa naishi awali huyu mama alikuwa na mapacha watatu jamani nilipenda kwenda kuwabeba nikifika na zawadi vinaanza kuniita amaa amaa amaaa.

Kitoto cha mdogo wangu dah huyu ndo funga kazi yaan kinanipenda utafikiri mm mdo mama yake aliwa mdogo kuna kipindi nililazimika kuishi nae basi nilipenda kumuimbia hili alale basi nitaimba nyimbo za kiruga mpaka asinzie.

Siku moja alinichekesha alikuta nimelala hapo kashakuwa 3yrs akasema "mama imbia wewe" nikasem imba" akaanza baby oh nana nana baby! Hapo ananipiga mgongoni nilicheka sana. Watoto watam
 
Malezi duni mkuu, unajua watu wanadhani kumlea mtoto ni kumlisha, kumsomesha na kumvalisha wanasahau kuwasimamia na kuwaongoza watoto kwenye njia sahihi, wanawaacha watoto watazame chochote kwenye TV na kwenda kucheza kwenye mazingira ambayo si rafiki kwa akili ya mtoto na matokeo yake ndio hayo. Kwa mfano mtoto wa huyo mzee aliridhika kwa sababu aliona babake ana maisha mazuri na kitendo cha kukaa naye ofisini kilimjengea mtoto mtazamo wa uhakika wa kula bila jasho ndio maana mzee wake amemuona hayuko kama alivyotegemea.

Haiba ya mtoto haichangiwi na malezi tu jamani. Unaweza kumlea mtoto kwa bidii zote na bado akakutisha tamaa. Malezi ni kipengele muhimu lakini kuna uzoefu binafsi wa mtoto, mazingira yanayomzunguka na tabia zingine zilizoko kwenye "damu" yake zinazomtofautisha na watoto wengine. Unaweza kuwa na watoto sita lakini wakawepo watatu au mmoja yuko tofauti kabisa na wengine. Watoto pamoja na malezi tunayowapa nao wana chaguzi zao. Kuna watoto walikuwa wakienda shamba au ofisini na wazazi wao na wakavutiwa na kuazimia kuja kuwa kama baba au mama na wakawa na wengine wakaazimia wakashindwa. Nina babu yangu ana watoto saba. Yeye na mkewe ni wasomi na wana uwezo mkubwa mpaka leo maana waliwekeza vizuri ujanani. Watoto wake sita ni wasomi na wana familia zao na shughuli nzuri za kuwaingizia kipato. Mmoja pamoja na bidii zote za wazazi hakuna kilichowezekana. Mpaka leo yuko 40s anakaa na wazazi wake; amekuwa tu dereva wao. Sasa sijui walikosea nini kwa huyo mmoja. Bahati pia inahusika kufanya mtu awe alivyo.
 

Ebooo...!! Suruali ngapi zinatembea barabarani daily ..?? Hazikataagi mitongozo halafu., Kwa nn usijikwapulie mmoja mkazaa..??
[emoji15] kwani unazaa tu na suruali yoyote?
 
Wa kwangu ana 1.1 ni wa kiume. Anajua vzr kutamka neno "acha" kutokana na fujo zake za kuvurugavuruga vitu. Tumejikuta tunamkataza amelishika hilo neno. Siku hizi hata akiniona mm au mama yake vitu kama kioo nk. Utamsikia na yeye anakuambia "Acha" huwa tunacheka sana.
 
Hahahaaaa nampenda sana mwanangu, na huwa nawaambia watu watoto wa uzeeni ni watamu sana[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Anamiezi kumi meno matano, ndo anatembelea vitu ila mjanja sana hapendi umgombeze anakunja USO,
Wakati meno yanaota alikuwa ananing'ata sana namwambia ntakuchapa huku namchapa kweli, sasa umekuwa wimbo wake mda wote anaimba "anchabang', mara chabaa, ataa(achaa), akimwona mtoto anaita Toto, hata kama ni yy anajiangalia kwenye kioo.

Kinachoniachaga hoi babake akiwepo halali ancheza tu mpaka saa4,5 hadi 6 usiku[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]huwa namwambia mwanangu unawivu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nampenda sana, ila nabalance mapenzi kwa baba na mtoto
 
Wangu mm ana 4 years yani yeye akiamka asubuhi Tu ni kuwasha laptop na kuanza kuangalia katuni hata Kula anasahau ,simu ya mamake ndo anaimiliki muda wote yy ni kuangalia katuni tu

Kwani haendi shule? Ulivyolielezea ni kama imekuwa tabia sugu. Sasa kama ana miaka minne yuko hivyo akifika sita utaweza kumgeuza? Uzoefu na tafiti zinaonyesha watoto wanaodamkia na kuchezea hivyo vitu muda mwingi au mara kwa mara wanakuwa wazito shuleni na mwilini. Lap top ikae mbali awekewe ratiba ya kuangalia katuni kwa muda mfupi tu kwa siku au siku kadhaa za wiki. Nani alimwambia dunia iko hivyo? Kwamba ukiamka kitu cha kwanza ni kucheza??? Lazima ajue maisha yana utaratibu - kuna kusali kama mna dini, kufanyia mwili usafi, kula chakula kwa nafasi bila kuingiliwa, kucheza michezo inayohusisha viungo vya mwili pamoja na watoto wengine, kupeleka vikombe jikoni n.k. Hiyo simu hata mkiweka password ataing'amua. Ikae mbali na akataliwe kuichezea hata kama atajipigapiga ukutani. Mtoto wangu nimekuja kupata tabu sana kumkomesha simu kwani utotoni nilikuwa naona sawa tu lakini alivyokuwa mkubwa nikaona madhara yake. Ukirudi nyumbani anataka simu, akija mgeni anataka simu yake, akishika simu yako itamchukua dakika 10 kukupa toka ulipoitaka, ukimuita hasikii, anakuwa anajua vitu vingi kwenye simu kuliko wewe maana anapata muda mwingi wa kupitia na kujaribu. Hii ni mbaya kwa sababu wewe unatakiwa udhibiti anachocheza au kuangalia. Sasa kama hata hujui ni nini unabaki tu kumuita akutolee unapoteza nafasi yako. Nashauri wazazi wenzangu tuweke gadgets mbali na watoto.
 
Mi wa kwangu balaa natamani akue kidogo labda nitapata zuri la kueleza, leo ni wiki ya tatu sijalala nakesha, dogo analala mchana wakati mimi nipo job, usiku halali na akilala mikononi ukimuweka kitandani tuu yani kabla hata hujakiacha kitanda kishaamka na kelele nyingi, kingine asee usikae karibu na mamaake ugomvi wake c mdogo atalia hapo hadi utashangaa, kingine tangu wiki iliyopita hajacheka sijui ndo kutabasamu hakuna. Ana miezi 4. Hataki kulazwa kama watoto wengine anapokuwa macho, yeye anataka kukaa na anakaa...huyo ni mdogo, kakayake yeye anapenda ngumi, anajua bunduki zote kwa majina, hili nimejaribu kumuonya mamayake asiwe akimuwekea movie za mapigano zaidi ya cartoon lakini sijui huyu kijana anajifunzia wapi maana hakawii kukwambia anataka awe mwanajeshi sababu hapendi majambazi, huyo Ana miaka mi 4, anajua kikorea, kajifunza wapi mi sijui...ila ana shida moja anapenda tambi tuu, vyakula vingine kula mpaka mpigizane kelele sana na husingizia anataka kukojoa akienda harudi..ana huruma sana na mamayake, mjanja mjanja sana ukikasiririka atajua jinsi ya kukufanya ucheke tuu, shida usimuache na mdogo wake peke yao, unaweza kuta mtoto analishwa ugali.
Hahahaaaaa nimecheka sana. Yeye hataki ugali lkn anamlisha mdogo wake [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Watoto wanaongeza upendo ndani ya nyumba
Ni kweli maana unawezakuta umevurugwa na mkeo alafu dogo anakuja baba babaaa, unashindwa kununa maana anataka mcheze na automatically unajikuta yale makosa umesamehe[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom